Somo la 1/21

Ukurasa wa 4/5: Mada B: Zoezi la kwanza katika programu

Mada B: Zoezi la kwanza katika programu: Maarifa yako binafsi kuhusu uhusiano wa karibu na kutenganishwa

Katika somo hili zoezi la kwanza litakusaidia kutambua maarifa yenye manufaa ambayo tayari unayo kuhusu namna watoto wanavyoonyesha hisia wanapotenganishwa na walezi. Hii itakusaidia kuelewa namna unavyoweza kutumia uzoefu wako wa maisha kama maarifa katika kuelewa na kufanya kazi na mtoto anayelelewa.

Mahojiano kati ya wazazi walezi, au kati ya wazazi walezi na msimamizi:

  • Madhumuni ya mahojiano ni kujua unafahamu nini kuhusu uhusiano wa karibu na watu muhimu unakua, na pia jinsi ulivyoonyesha hisia katika kutenganishwa nao wakati unakua. Licha ya kujadili namna kila mzazi mlezi anavyoweza kutumia uzoefu wa utoto wake anapofanya kazi kama mtaalamu mlezi wa mtoto.
  • Mshiriki mmoja anamuhoji mwingine kwa dakika 20.
  • Kisha dhima zinabadilishwa na mtu mwingine anahoji.
  • Baada ya mahojiano, mtatafakari kila mmoja kuhusu maarifa yako.

Uliza tu maswali na sikililiza majibu. Tafadhali usimkatishe mtu anayejibu, sikiliza kwa makini.

MAHOJIANO

Mwanzo wa maisha yako: 

  • Hali ya wazazi wako ilikuwaje wakati mama yako alipopata ujauzito – waliishi wapi, walikuwa na umri gani, walikuwa na watoto wangapi?
  • Je, unajua ujauzito wa mama yako ulikuwaje na kuzaliwa kwako? (je, wazazi wako walikwambia hadithi zozote kuhusu hilo?)
  • Nani alikutunza tangu kuzaliwa kwako hadi ulipofikisha umri wa miaka 3?
  • Ni njia ipi ya kimila ya kulea watoto katika utamaduni wako?
  • Kitu gani kilikuwa kizuri katika namna wazazi wako walivyokulea?
  • Hili lilikupa thamani gani katika maisha ya familia?
  • Ni hali gani yenye ulinzi na kufariji zaidi unayoweza kukumbuka katika utoto wako na mzazi au mlezi?
  • Ni kutenganishwa kupi kwa mara ya kwanza kulikuwa kugumu unakoweza kukumbuka, muda mrefu au mfupi?
  • Ulionyesha hisia gani kwa hilo – ulifikiri, kuhisi au kufanya nini?
  • Ulijaribu vipi kumudu na kutenganishwa huko – ulifikiri, kuhisi na kufanya nini? (hasira kwa mlezi?, “ulikaa nalo kimya?”, ulijaribu kusahau au kupuuza na kuendelea na kazi?, ulijisikia huzuni?
  • Ni mambo gani yalikuwa ya msaada zaidi waliyofanya watu wazima kukusaidia kupitia wakati mgumu wa kutenganishwa?


Maendeleo yako kitaalamu:

  • Kitu gani kilikufanya uchague kuwa mzazi mlezi?
  • Kwa kuzingatia uzoefu wako wa utotoni: Ni maadili yapi ya msingi ambayo ni muhimu sana kwako kama mlezi mtaalamu – ni kitu gani muhimu sana kwako katika matunzo ya mtoto?

Maendeleo yako kitaalamu:

  • Unajisikiaje kuhusu mtoto wako unayemlea?
  • Ni jambo gani uliloona zuri na gumu sana katika kazi yako ya kila siku?
  • Je, unatambua lolote kati ya matatizo ya mtoto kutokana na utoto wako? Je, uelewa huu unaweza kutumikaje katika namna unavyofanya kazi na mtoto?
  • Unafikiri ni kitu gani ni muhimu sana kwako kukifanyia kazi ili kuwa mlezi mtaalamu mzuri?