Somo la 1/19

Ukurasa wa 5/5: Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Mwishoni mwa kila somo unaamua kuhusu mpango kazi. Kwa mpango kazi wa kwanza, tunapendekeza kwamba;

  • Tengeneza video ndogo ya mazingira ya kila siku na mtoto kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kama huna simu, tafuta tu mazingira ya kila siku, fuatilia na kumbuka ili uweze kuyaeleza katika masomo ya mafunzo yanayofuata. Kwa mfano, kupata kifungua kinywa pamoja, kufanya kitu kinachofurahisha, kufanya kazi n.k. Hakikisha unajumuisha watu ambao mtoto anajumuika nao katika uangalizi wako au kurekodi video.
  • Video hizo au uangalizi zitakuwa ni vitu vyenye thamani kubwa kwa mtoto siku moja atakapoondoka katika malezi yako.
  • Unaweza kujadili na kutafakari kwa pamoja ulichokigundua na namna unavyotoa matunzo ili kuelewa kipi kinafaa na kipi hakifai kwa watoto walio katika matunzo yako.

Wazazi walezi wanachukua filamu ya hali ya kila siku na watoto wao wanaowalea

Asante kwa utayari wako na kila la heri katika kazi yako hadi somo linalofuata!