Somo la 10/19

Ukurasa wa 3/7: Mada A: Kukosa kundi lenye msingi salama mtoto anapowekwa mbali na nyumbani

Mada A: Kukosa kundi lenye msingi salama mtoto anapowekwa mbali na nyumbani

Kwa nini uzingatiaji wa leo ni muhimu?

Wakati mwingine, watoto na vijana katika malezi hawakumbani na utenganishwaji kutoka kwa wazazi wao tu. Pengine wamekabiliwa pia na upotezaji mwingine wa watu na utenganishwaji kabla ya kukutana na wewe. Huenda wamewekwa kwenye familia kadhaa walezi, kuishi na ndugu, au katika makazi ya watoto ambako walezi wamebadilishwa mara nyingi. Pia wanaweza kuwa wamekutana na migogoro mingi baina ya wazazi kama vile talaka, kugombea kuwa waangalizi, n.k. Watoto wanapokosa uhusiano salama na wa muda mrefu wa mlezi, wanaonyesha hisia kwa kuwa na tabia ya kuonyesha uhusiano usio salama (kama ulivyojifunza katika somo la 9: kujitenga, ukinzani na kutokuwa na mpangilio). Wanapoingia katika familia mlezi, wanaweza kuonyesha ugomvi, kujitoa au uhusiano wa kibaguzi katika kuchanganyika kwa kila siku. Inaweza kuwa vigumu kwao kuelewa waseme au wafanye nini, na namna ya kuwaheshimu wengine katika familia. Huu unaweza kuwa ni uzoefu unaosumbua sana kwa wanafamilia wote, pia kwa mtoto anaweza kuhisi kukataliwa anaposhindwa kuelewa na kutumia maadili ya mwenendo wa jamii ndani ya familia.

Kwa hiyo, anahitaji kufikiri sana, mazungumzo na mipango ndani ya familia mlezi ili kukabiliana na matatizo hayo ili kutafuta njia mpya za kufanya uhusiano wa kijamii ufanye kazi, na kumfanya mtoto ahisi kwamba ni sehemu ya familia na ana uhusiano. Kwa sababu hiyo kumfanya mtoto kuweza kujifunza polepole jinsi ya kuchangamana kila siku. Mara nyingi, inachukua jitihada kubwa na za uvumilivu hadi shughuli za mipaka na majukumu zifanye kazi kwa wanafamilia wote, wakiwemo watoto wa familia mlezi.

Lakini hata watoto wanaotoka katika mazingira magumu wanaweza kujifunza hilo. Pia wanaweza hata kuwa mawaziri wakuu kama watapata msaada wa subira kutoka kwa wazazi walezi na wataalamu.

 

WATOTO KATIKA MALEZI WANA CHANGAMOTO ZIPI, NA KITU GANI KINAFAA UNAPOJARIBU KUWASAIDIA?
Katika tafiti za vijana waliokulia katika taasisi na familia walezi, mara nyingi wanaeleza hisia za kutojitukuza, kukataliwa, na kutokuwa na makazi. Pia wanahisi kwamba watu wachache sana katika jamii wanazungumza nao kuhusu hasa kilichotokea: haja yao ya kuwa na watokako. Katika tafiti za vijana wasio na makazi, wengi wao wamekulia kwenye taasisi au katika ulezi. Ukuaji huu wa huzuni katika matukio mengi unaweza kuzuiwa katika famila mlezi kwa kumfanya mtoto ajisikie kujumuishwa na kujenga ujuzi wake wa kijamii.

Wazazi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Danish Anker Jorgensen walifariki akiwa na miaka mitano. Katika mapendekezo yake kwa Fairstart, alieleza kwamba mafanikio yake katika siasa yalitokana na malezi kutoka kwa shangazi yake ambaye alikuwa mama yake mlezi. Pia kwamba makazi ya watoto ambako alikulia baadaye katika maisha yalikuwa na mvuto mkubwa wa kijamii.

 

Watu wazima, ambao walikulia katika mfumo wa malezi, ambao wamefanikiwa katika utu uzima wote wanaeleza sifa nne za walezi wao wa utotoni:

 

  • Mlezi mmoja au wawili mahususi waliwajali katika maisha yao na kuwaruhusu kujenga nao uhusiano wa karibu. Watu hao walikuwa wavumilivu na kuwapa muda wa kukua taratibu.
  • Waliweza kupewa sehemu binafsi ya kwao wenyewe.
  • Waliishi katika kikundi (familia mlezi au taasisi) ambako walijifunza ujuzi wa kijamii ambao hawakuwa wamejifunza kutoka kwa familia zao halisi.
  • Kundi lilikuwa na uhusiano mzuri na mtandao wa eneo husika, na kumfanya mtoto kukubalika katika jamii.