Somo la 10/19

Ukurasa wa 6/7: Mada D: Kuboresha uhusiano katika mtandao wa familia mlezi

Mada D: Kuboresha uhusiano katika mtandao wa familia mlezi

Tabia ya watoto na vijana ambao walitelekezwa mara nyingi huleta kutokubaliana kati ya wanafamilia katika mtandao wa familia mlezi: familia ya wazazi walezi, shule, labda shule ya awali. Inaweza kuwa vigumu kufanya pande zote zimuelewa mtoto, tabia yake na namna hili linavyoweza kufanyika. Kutokubaliana kunaweza kutokea kwa sababu mtoto anaweza kuwa na tabia tofauti sana katika mazingira tofautitofauti.

Pengine mtoto ana matatizo ya kuwa katika uhusiano wa karibu na wa ndani, hivyo mara nyingi anachanganyikiwa na kuwakasirikia wazazi walezi, lakini anaweza kutokuwa na matatizo hayo kwa mfano, shuleni, ambako kuna utaratibu zaidi na hakuna mahitaji mengi ya kihisia. Au anaweza kufanya kazi vizuri katika mazingira madogo na utaratibu wa kila siku katika familia mlezi, lakini anachanganyikiwa na kutokuwa na utaratibu mzuri kama kuna watu wengi, kelele nyingi na walimu wengi shuleni.

Hivyo, kwa mfano, ni kawaida kwamba wazazi walezi na walimu wa shule wanaweza kuwa na maoni tofauti kabisa na labda kutokubaliana kuhusu anavyovitaka mtoto. Aidha, ndugu wa wazazi walezi wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusiana na mtoto huyo: “Una msimamo mkali sana” au “unamjali zaidi yeye kuliko watoto wako”, au “sina matatizo na yeye, kwa nini wewe?”.

Hapa, familia mlezi kutokana na mfano wa kwanza wanaelezea namna walivyofanya ili mtandao wa wanafamilia wamuelewe mtoto wao wanayemlea na kushirikiana naye:

Alikuwa akiwafurahia watu wageni wakati wote, na alikuwa karibu na kila aliyekutana naye – hata watu wa mtaani ambao hakuwajua kabisa. Watu wakati wote walijibu kwa kusema alikuwa ni mvulana mzuri sana duniani, na kutulaumu kwa kuwa wakali kwake. Lakini kama akikaa na mtu mmoja kwa muda mrefu, kama alivyokaa shuleni, matatizo yake yalijitokeza wazi. Alikuwa na hali ya hamaki, aliwachokoza watoto wengine, hakuweza kukaa kwa utulivu na alibishana na mwalimu wake kuhusu hata uamuzi rahisi tu. Baada ya muda mfupi mwalimu wake alianza kusema kwamba hatukujua namna ya kumlea. Hali hii inatokea wakati wote kwa watu wageni: awali wanampenda na kisha wanashangazwa na tabia yake katika mazingira ya ukaribu sana. Baada ya majadiliano mengi pamoja na sisi, alianza kuelewa matatizo ya watoto waliotelekezwa na hatimaye tunaweza kushirikiana. Tuliandaa mpango wa namna ya kumkabidhi asubuhi na namna ya kuelezana haraka kunapotokea matatizo. Sasa tunashirikiana vizuri sana. Anajua kwamba tunashirikiana na kwamba yuko salama na anasaidiwa wakati wote”.

MASWALI KWA AJILI YA KUTAFAKARI NA MAZUNGUMZO

Dakika 10

  • Je, unatambua matatizo kati ya walezi na mtoto wako unayemlea?
  • Je, umekutana na changamoto gani katika kumfanya kila mmoja katika mtandao kuelewa tabia ya mtoto katika hali tofauti?
  • Je, una uzoefu, mawazo au mapendekezo ya namna ya kuwafanya watu katika mtandaokufikiria na kutenda kwa pamoja?

 

ORODHA YA MAMBO YA KUELEWA
  • Kwa nini watoto na vijana wanaopelekwa nje na nyumbani mara nyingi kujitambua kwao kupo chini na wanajisikia kuwa hawana mahalipa kuishi?
  • Je, utamfanyaje mtoto ajisikie kuwa ni mmoja kati ya familia mlezi, na ana nafasi yake mwenyewe?
  • Je, utafanyaje kumsaidia mtoto ajifunze kuhusu mazungumzo ya kila siku na jinsi ya kujibu katika hali za kila siku?
  • Uzoefu wako ni upi katika kumfanya kila mmoja kumuelewa mtoto katika namna moja? Utafanyaje kuendeleza hili?