Somo la 10/15

Ukurasa wa 1/7: Kuhimiza kujenga uhusiano kwenye kazi kwa vitendo

Kuhimiza kujenga uhusiano kwenye kazi kwa vitendo

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

  • Kuimarisha hisia ya mtoto ya kuwa na nafasi binafsi ya inayoonekana na ya kijamii kama msingi salama wa kujenga uhusiano katika familia mlezi.
  • Kuwafanya watoto waliowekwa kwenye matunzo kuhisi kwamba wao ni sehemu ya familia na kuwasaidia kujifunza namna ya kuenenda katika maisha ya kila siku ya familia.
  • Kuwahusisha wanafamilia wote katika kujua wajibu wao na mipaka yao kama wanafamilia wa familia mlezi.
  • Kushirikiana na mtandao wa familia mlezi ili kuzifanya pande zote kukubaliana kwa pamoja kuhusu mahitaji ya mtoto, na jinsi ya kumfanya mtoto ajishughulishe.

Mada ya somo:
Katika somo la 6 (Jinsi ya kutoa Matunzo ya Kitaalamu) ulijifunza namna ya kujenga uhusiano wakati unafanya kazi zako za kila siku za vitendo. Pia ulijifunza namna ya kuwahusisha watoto katika kazi za kila siku na kujumuika nao wakati ukifanya hivyo. Katika somo hili tunaangalia namna ya kusimamia ujumuikaji na jinsi ya kumfundisha mtoto kuhusu mipaka na wajibu.

Mara nyingi, watoto na vijana wanaotunzwa wanaweza kuhisi kwamba hawana mahali wanakotoka. Wanaweza kukosa hisia ya mipaka ya mahali na hisia na kukosa uelewa wa wajibu na mipaka katika maisha ya kila siku ya familia mlezi.

Watoto wengi walio katika matunzo hawajifunzi katika maisha yao ya utoto namna ya kutenda katika uhusiano, na namna ya kufuata utaratibu wa kila siku katika familia. Wanahitaji msaada ili kujenga hisia ya mipaka. Unachokifanya na usichokiongelea, na lini na wapi? Unajifunzaje kuheshimu mipaka ya sehemu na jamii?

Kwa mfano, je, mtoto anaweza kuchukua kitu cha mtoto mwingine bila ya kuomba? Je, mtoto anatambua kwamba lazima asaidie kutayarisha chakula, au kufanya kazi zake za shule nyumbani? Je, tunaongeleshana kwa sauti ya juu au sauti ya utulivu? Hii ni hatua ya kujifunza, kwa mtoto pamoja na kwa wanafamilia wote wa familia mlezi.

Ndani ya mtandao wa familia mlezi, mtoto anaweza kuwa na mwenendo tofauti sana katika mazingira tofauti (kwa mfano: migogoro mingi nyumbani, hakuna migogoro shuleni au kinyume chake). Kwa sababu ya hilo, mtoto anaweza kutizamwa kwa utofauti sana katika mtandao wa watu wanaowajibika kwa mtoto (wazazi walezi, mwalimu, mwelimishaji). Kunaweza kuwa na kutoelewana sana katika namna mtoto anavyojishughulisha na namna kulishughulikia hilo. Ni namna gani wazazi walezi wanafanya kuhimiza makubaliano ndani ya mtandao kuhusu mahitaji ya mtoto au kijana.

 

Malengo ya somo:
Kusaidia ukuaji wa kijamii wa mtoto katika kuchanganyika kwake na watu kila siku. Kuitia moyo familia mlezi katika kutafuta wajibu na njia mpya za kuweka mipaka wakati mtoto mgeni anapoingia kwenye familia, ili wanafamilia wote wahisi kuarifiwa na kuheshimiwa. Kujenga uelewa wa pamoja wa mtoto na mahitaji yake katika mtandao wa eneo analoishi mtoto.