Somo la 11/19

Ukurasa wa 3/4 Kuwasaidia watoto kuelewa historia zao mbalimbali - Mapendekezo kwa ajili ya mazoezi.

Kuwasaidia watoto kuelewa historia zao mbalimbali – Mapendekezo kwa ajili ya mazoezi

A. KUTAKA, NA KUWEZA, KUTOA HUDUMA NI VITU VIWILI TOFAUTI
Njia ya kitaalamu ya kuonyesha heshima kwa wazazi wa mtoto inaweza kuongelewa na mtoto kwa namna hii:

“Nina uhakika kwamba wazazi wako muda wote wamekuwa WAKITAKA kukuhudumia vizuri. Lakini cha kusikitisha si wazazi wote WANAWEZA kuwapa watoto wao mapenzi wanayotaka kuwapa, hata hivyo wengi wanataka kufanya hivyo. Hata kama wanakupenda, unajua wazazi wako wana matatizo mengi katika maisha yao wenyewe (unaweza kutoa mifano ambayo mtoto anaweza kutambua, kama vile,” Mama yako alianza kunywa pombe tangu akiwa mtoto, na sasa hawezi kuacha kunywa hata ajitahidi vipi”). Hii ndiyo maana walifanya kitu cha kuwajibika sana na waliamua kitu kigumu sana kwako: kuwaomba wengine wakupe huduma nzuri wewe! Pengine hawakuomba moja kwa moja, lakini kwa kuonyesha matatizo yao kweli walikuwa wanaomba msaada wa kukuokoa –kitu hiki kilikuwa kigumu kwao kukisema moja kwa moja. Kwa hiyo wazazi wako walijitahidi sana kufanya kile kilicho bora kwa ajili yako. Hata kama wana hasira au wivu dhidi yetu na kutaka kukuchukua tena, tunajua hii inamaanisha kwamba wanakupenda, na ni vigumu kuwaachia wengine wakuhudumie. Wanajua kwa kina kwamba pia ni vigumu kwao, lakini wanakuonyesha kwamba wanataka kukuhudumia. Hatuna hasira nao pale wanapofanya hivi –tunajaribu kuwasaidia wao kwamba wamefanya uamuzi sahihi kutuomba sisi tukuhudumie”

B. “UNA JOZI MBILI ZA WAZAZI UNA BAHATI!”
Kumsaidia mtoto kuelewa hali yake, maelezo haya hutoa mtazamo usio na migogoro kati ya wazazi walezi na wazazi asili:

“Unajua una bahati – una mama wawili ambao wanataka kukupa maisha mazuri, na una baba wawili ambao pia wanataka kukupa maisha mazuri. Wazazi wako walifanya jambo la ajabu: walikuzaa wewe, na ulikuwa tumboni mwa mama yako kwa miezi tisa. Wazazi wako walipochoka ulikuja kwenye ulezi wetu. Hivyo kwa njia hii una wazazi wanne waliokubali kukuhudumia. Kile ambacho mmoja wetu hawezi kufanya wengine wanaweza kufanya. Ikiwa wakati mwingine hatutakubaliana, ni kwa vile tu sote tunataka kukuhudumia kadri tunavyoweza”.

C. KUTENGENEZA ‘FUMBO LA VYANZO VINGI” KUWA WAZO MOJA LA UTAMBULISHO

Kwa zoezi hili unahitaji mkasi, tepu, karatasi kubwa na penseli au kalamu za rangi mbalimbali. Unaweza kutumia vifaa vingine kama vinawapendeza watoto zaidi, kama vile vipande vya mkate, au majani ya miti, au vitu vingine utakavyoona vinafaa. Kila kifaa kitawakilisha mtu ambaye ana uhusiano au alikuwa na uhusiano na mtoto.

Zoezi linaweza kufanywa na watoto wa kuanzia miaka mitano mpaka kumi na mitano. Linaweza kufanyika katika mchana wa siku moja au mbili, na linaweza kurudiwa mtoto anapokuwa mkubwa na kuelewa zaidi kuhusu hali yake.

Kwanza mwambie mtoto (au msaidie) kuchora “Watu wote ambao wamewahi kukutunza” katika makundi tofauti kwenye karatasi. Kila kundi linapaswa kuwa na rangi yake, jina au aina nyingine ya kiashirio.

Wanaweza kuwepo babu na bibi, wazazi, ndugu, walezi katika maeneo ya awali, mkunga na daktari aliyesaidia wakati wa kuzaliwa, wazazi walezi na watoto wao, mbwa au paka ambaye mtoto yuko karibu naye, jirani, watoto wengine wanaolelewa kwenye familia hiyo, watoto anaosoma nao, n.k. Tumia muda wako kumsaidia mtoto kuandaa namba ya makundi anayoweza kuyaacha. 

Kwa kila kundi, chagua baadhi ya maswali yafuatayo na muulize mtoto. Mwambie mtoto atafute neno moja kama jibu. Chochote anachojibu mtoto, andika neno au alama chini ya kundi linalohusika.

  • “Una kumbukumbu gani nzuri kuhusu mtu huyu au (watu hawa)” (Andika neno/alama).
  • “Ni jambo gani zuri sana kuhusu mtu huyu?”(nywele nzuri/sauti nzuri, upendo, ukarimu, ana nguvu, nk.)
  • “Ni kitu gani kizuri sana ambacho mtu huyu alikufanyia wewe?” (Alikuzaa, anakumbuka siku yako ya kuzaliwa, nk.)
  • “Ni kitu gani kinakufanya ucheke kuhusu mtu huyu – ni kitu gani cha kuchekesha kuhusu yeye?” ( kwa mfano: namna anavyotembea, vitu vya hovyo anavyosema, tabia ndogondogo za ajabu, n.k.)
  • “Ni kitu gani kizuri ulichopokea kutoka kwa mtu huyu” (ujasiri, nguvu, ustahamilivu, afya njema, nywele nyekundu, nk.)
KUJAZA FUMBO HILI LA “MIMI NI NANI?”
Baada ya hapo, chukua karatasi la gazeti na muombe mtoto (au msaidie) kuchora taswira ya umbo lake ambayo ni kubwa sana ambayo inajaza karatasi yote. Mwambie mtoto kuweka jina lake au alama kwenye taswira na sema:

Sasa tutaangalia wewe ni nani! Tuko kama tulivyo kwa kile ambacho wengine wamekuwa wakitupa katika maisha. Tuko kama magari madogo yaliyo wazi nyuma ya kubebea mizigo ambapo tunachukua kila kitu kizuri wanachotupa watu. Kutafuta wewe ni nani ni kuangalia wengine wamekupa nini, na inaonekana walikupa zawadi nyingi za ajabu! Umeshakutana na watu wengi katika maisha yako, kwa hiyo ni fumbo kamili tunakwenda kutengeneza sasa!”

Kama unatumia vifaa kama vipande vya mkate, mawe, majani au vitu vingine, unaweza kuweka kipande katikati na kusema: “Huyu ni wewe na gari lako aina ya pikapu. Sasa, hebu tuangalie vitu vizuri vyote walivyokupa watu na viweke kwenye gari. Kisha tunaweza kuona namna ulivyo mzuri na mwenye nguvu! Kipande hiki ni bibi yako ambaye alikuwa mkarimu sana – hebu tumuweke kwenye gari, na unakuwa mkarimu! Huyu ni mbwa anayekupenda sana – hebu tumuweke mbwa kwenye gari lako ili ujisikie upendo. Na kuendelea. Fanya hivyo kwa watu wote ambao mtoto amewataja.

Kama unatumia karatasi na penseli:

Sasa chukua karatasi ya kwanza yenye makundi na sifa na mwambie mtoto aweke kipande cha picha kwenye kila kundi ikijumuisha maneno/alama kwa ajili ya kila kundi na weka riboni/kinasa sauti “sehemu ya fumbo” kwenye taswira ya umbo lake. Mtoto lazima aweke makundi au watu kwenye taswira ya umbo lake pale panapostahili. Kwa mfano kama mtu amempenda, kipande lazima kiwekwe karibu na moyo wa mtoto. Kama mtu alikuwa msikilizaji mzuri, weka kipande hicho kwenye masikio, n.k.

Mtoto au wewe unaweza kurekebisha vipande vya picha wakati unaviweka ili vifae vizuri kila kimoja kama kwenye vipande vilivyo kwenye fumbo. Unaweza kutoa maoni kuhusu jambo hili, kwa mfano: “Ni wapi unafikiri sisi wazazi walezi tunapaswa kuwekwa na wapi unafikiri familia yako inapaswa kuwekwa? Labda kama tukibandika kipande kidogo cha wazazi walezi, je, kitakaa vizuri na wazazi wenu?” Kwa njia hii unaweza kumsaidia mtoto kujenga wazo la wazazi na wazazi walezi “kuwakwa mahali pamoja”.

Baada ya mchakato wa kupanga vipande kwa pamoja, unaweza kuelekeza uzingativu wa mtoto kwa “Mimi ni nani basi?”:

Sasa unaweza kuona vitu vyote vinavyoweza kuwekwa pamoja katika wewe ni nani! Wewe ni Jack, na unafurahisha, una nguvu, una tabasamu kubwa, ni mkimbiaji mzuri sana, unajua jinsi ya kuaga usiku kwa kukumbatia (au alama na maneno yoyote kwenye taswira ya umbo yanavyoashiria). Ninyi nyote ni vitu vizuri ambavyo watu wamewapa, na vyote ni sehemu yenu sasa! Wewe ni mtoto wa mwenye bahati sana”.

Kisha unaweza kutundika mchoro huo katika chumba cha mtoto au jikoni ambako anaweza kuiona kila siku na endelea kufanya mazungumzo na mtoto kuhusu mchoro huo. Unaweza kugundua kwamba marekebisho yanahitajika, ambayo unaweza kujadili na kutekeleza.

D. KUTAFAKARI KUHUSU MCHAKATO WA KUTENGENEZA UTAMBULISHO 

Kwa watoto wakubwa (kuanzia miaka 10 na kuendelea) na vijana, video hii inaweza kuwa zoezi ambamo unaweza kumwona mtoto kwa ujumla. Kisha unaweza kuwa na mazungumzo kuhusu nini alichosema Yusta katika filamu hii- na namna alivyotengeneza utambulisho binafsi kutokana na uzoefu wake wa walezi tofauti katika maisha yake Katika mchakato huu unaweza kujadili na kijana namna anavyotafakari mada iliyowasilishwa na Yusta: Walezi tofauti aliokuwa nao, utenganishwaji, namna uzoefu unaofanana na huo ulivyomwathiri mtoto anayemlea, namna mtoto huyu anavyojaribu kuendana na hili na kuunda maoni binafsi kuhusu yeye mwenyewe na wengine.

F. MSAIDIE MTOTO WAKO UNAYEMLEA KUTUNGA HADITHI YAKE YA UTAMBULISHO
Baada ya kuona na kujadili video hii kwa pamoja, unaweza kumhamasisha mtoto au kijana kusimualia au kuandika hadithi kuhusu watu wote waliomuonyesha upendo, uwezo, watu waliomfanya acheke, n.k.
Kama una kamera unaweza kuchukua video inayofanana. Hii inaweza kuwahusu watu ambao mtoto amekuwa na uhusiano nao. Mtoto anaweza kueleza anajisikiaje kuwa na vyanzo tofauti vya asili. Hii inajumuisha hatua ya kukubaliana na kuwa na familia mbili. Zungumzia kuhusu vipengele vyote vizuri na vya kufurahisha vya kupata uzoefu mwingi katika umri huo mdogo.
LENGO LA MAZOEZI HAYA
Lengo la Mazoezi haya yote linafanana:
Kumwonyesha mtoto kwamba unakubali vyanzo vya asili yake, kwamba uko tayari kuwa na mazungumzo kuhusu wao na matatizo yanayohusiana na kuwa na vyanzo vingi vya utambulisho.
Pia, kwamba watu wote tofauti aliokutana nao wametoa kitu fulani kizuri, na kwamba vitu hivyo vizuri ni sehemu ya jinsi alivyo leo hii.
Ukijumuisha kumsaidia mtoto au kijana katika kutengeneza mawazo chanya kuhusu yeye mwenyewe. Mchakato huu ni endelevu kwa miaka utakayokuwa unamlea.