Somo la 12/15

Ukurasa wa 1/3 Kushirikiana na Mamlaka

Kushirikiana na mamlaka

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

Kutengeneza uhusiano wa kitaalamu na mamlaka.

Maudhui ya somo:

Katika masomo haya ya mafunzo utashughulikia uundaji wa uhusiano mzuri na mamlaka: wafanyakazi wa jamii, wasimamizi na mameneja wa familia mlezi.

 

Lengo la somo:

Lengo la somo hili ni kuelewa majukumu ya mamlaka na washauri ambao ni waajiri wako na kwamba unajiunganisha na vyama vya familia mlezi vya wenyeji katika nchi yako.

Ingia kwenye mtandao IFCO (International Foster Care Organization) www.ifco.info

Tafadhali tumia dakika 15 (au muda mwingi kwa kadiri unavyohitajika) kwa ajili ya kuhitimisha ulichokifanyia kazi kati ya somo la mwisho na hili la sasa:

•  Je, ulifanikiwa kukamilisha kile ulichokipanga?
•  Nini kilikuwa rahisi kukifanya na kipi kilikuwa kigumu?
•  Je, ulijifunza nini kwa kufanya ulichokipanga?
•  Kipi utafanya vizuri zaidi wakati ujao katika masomo?

Tafadhali kumbuka: Haina shida kama ulipata matatizo-hii ndiyo namna mpya ya kufanya kazi, inahitaji kufanyia mazoezi kabla haujazoea.