Somo la 13/19

Ukurasa wa 3/5 Mada A: Je, ni wazazi wa aina gani hasa ambao watoto wao wanapalekwa mahali pa kulelewa?

Je, ni wazazi wa aina gani hasa ambao watoto wao wanapalekwa mahali pa kulelewa?

Tafadhali angalia sifa hizi za wazazi halisi wa watoto wanaolelewa, na tafakari ni sifa ipi ya wazazi wa mtoto wako wako unayemlelea:
1. WAZAZI WA KAWAIDA AMBAO MAZINGIRA YALIWALAZIMISHA KUACHA KULEA
Wazazi ambao walikuwa walezi wazuri wanaweza kulazimishwa na mazingira na kuamua kuwa mtoto wao ni afadhali awe kwenye familia mlezi. Sababu ya jambo hili kwa kawaida ni:

A. Kina mama wanaolea peke yao ambao walifukuzwa kwenye familia zao kwa sababu walipata ujauzito kabla ya kuolewa, au kwa sababu walikuwa wadogo sana kutumia stadi zao kama wazazi.

B. Wazazi waliotatizwa na mazingira: kwa mfano kina mama waliobakwa, waathirika wa majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi, mafuriko, mdororo wa uchumi au kupoteza kazi zao, wazazi waliolemazwa na maradhi makali ya mwili, au kifo cha mzazi mmoja au wazazi wote wawili.

C. Familia ambazo mtoto alizaliwa akiwa na ulemavu mkubwa wa kimwili na/au alizaliwa kabla ya wakati au alikuwa na uzito mdogo na matatizo mengi wakati wa kuzaliwa.

D. Familia ambazo mama haonani na mwanaye– kwa mfano, mtoto anaweza kutengwa kwenye idara ya watoto wachanga, au anaweza kuwa amewekwa kwenye kifaa cha kukuzia watoto njiti kwa muda mrefu baada ya kuzaliwa. Kutengwa baada ya uzazi kunafanya iwe vigumu kwa wazazi wote kujisikia kuwa na uhusiano wa karibu na mtoto huyo, na mara nyingi husababisha kumkataa mtoto.

Tafakari yako kuhusu wazazi hao: Je, unafikiri wazazi wa mtoto wako unayemlea wanaendana na maelezo hayo kwa ujumla?

NDIYO:….. au HAPANA:…..

Kwa ujumla kushirikiana na wazazi, ambao walilazimishwa na mazingira kuwaacha watoto wao, inamaanisha wazazi hawa wana stadi za malezi na kwamba wanahitaji heshima yako na kuelewa hali yao.
Wazazi hawa mara nyingi wanaelewa ni kwa nini mtoto wao awe kwenye malezi na wataweza kuwasaidia.

2. WAZAZI WENYE MATATIZO
A. Mmoja au wazazi wote wawili wanaweza kuwa hawawezi kabisa kujihudumia maisha yao wenyewe, na pia wanaweza kuwa hawawezi kumhudumia mtoto wao katika njia salama na ya kiutendaji (ingawaje wanaweza kuwa bado wanampenda mtoto wao). Katika familia hizi mtoto aliye katika ulezi wako mara nyingi atakuwa na matatizo makubwa ya kuwa na uhusiano wa karibu na wewe kwa sababu alinyimwa malezi kama mtoto mdogo (unaweza kujifunza mada hii zaidi kwenye somo la 4 na 5).

B. Familia ambazo baba mara kwa mara nafasi yake inachukuliwa na baba wa kufikia (hii ni ishara kwamba mama hawezi kuwa na uhusiano wa muda mrefu kwa watu wazima na watoto pia). Familia ambazo baba ni mkatili kwa mke na watoto. Familia zisizo na baba ambaye anaweza kuwajibika kama mzazi.

C. Familia ambazo mama (au baba) mwenyewe alikosa na hakupokea malezi kama mtoto. Kihisia wazazi kama hao wanaweza kuwa wachanga sana na huwa wanafanya kama watoto kuliko wazazi: msukumo, wasioweza kukumbuka ahadi, wasioweza kupanga na kutekeleza kile kilichokubaliwa, kutokuwa na hisia ya namna gani aenende katika hali ya kijamii.

D. Familia ambapo walezi wa awali (kuanzia mtoto alipozaliwa hadi anafika umri wa miaka mitatu) walipata matatizo ya kiakili: mvurugiko wa akili, matatizo ya akili ya kubadilisha wakati, Matatizo ya akili yaliyosababisha usununu, huzuni kubwa ya muda mrefu baada ya kuzaliwa (unyongony’evu baada ya kujifungua), au wendawazimu wakati wa kuzaliwa. Kwa kifupi, mama au baba alisumbuliwa na magonjwa ya akili na kwa hiyo kushindwa kumtunza mtoto wake.

E. Familia ambayo mmoja au wazazi wote wana matatizo makubwa ya matumizi ya pombe au dawa za kulevya, na /au wamehusika na shughuli za uhalifu.

F. Wazazi waliokulia kwenye uyatima uliojaa umaskini sana muda mfupi baada ya kuzaliwa, na kupata matunzo kidogo kutoka kwa walezi wengi bila mpangilio. Baadhi ya maeneo ya kutunza mayatima yana wafanyakazi wachache na yana matatizo ya kuwatunza watoto katika hali salama na walezi wanaweza kuwa hawajihusishi na uhusiano wa kijamii na hisia na watoto hawa.

Tafakuri yako kuhusu wazazi: Je, unafikiri wazazi ( au walezi wa awali) wa mtoto wako unayemlea wanaendana na maelezo haya kwa ujumla?

NFIYO:….. au HAPANA:…..

Kwa ujumla kushirikiana na wazazi wenye matatizo ni changamoto kubwa kwa wazazi walezi. Kadri sifa zilizotajwa hapo juu zinavyoendana na wazazi wa mtoto unayemlea, ndivyo pia kunaweza kuwepo na changamoto ya ushirikiano na wazazi walezi. Wazazi wenye matatizo wana shida kubwa katika uhusiano wa kijamii, si tu kuwalea watoto wao, bali kwa kila uhusiano wa kijamii wanaokutana nao, ikiwa ni pamoja na uhusiano na mamlaka, familia zao wenyewe, na hata kwa familia mlezi.