Somo la 13/15

Ukurasa wa 1/5 Kushirikiana na wazazi halisi au ndugu

Kushirikiana na wazazi halisi

Tafadhali zingatia: Somo hili sio muhimu kwa kuwekwa katika matunzo ya ndugu – ni kwa ajili ya kutumiwa kwenye malezi tu.

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

•  Kuelewa umuhimu wa ushirikiano kwa maendeleo ya mtoto kwenye familia mlezi.
•  Kuelewa hali ya wazazi ambao mtoto wao yuko kwenye familia mlezi.
•  Stadi za kupanga na kutekeleza safari za kutembeleana na kuwasiliana kati ya wazazi walezi na wazazi halisi.
•  Kushughulikia hali ya matatizo kwa kushirikiana.

Maudhui ya somo:

Katika mafunzo haya utajifunza namna ya kushirikiana na wazazi halisi au ndugu wa mtoto ambaye yupo kwenye familia mlezi.

 

Malengo ya somo:

Lengo la somo ni kujifunza na kutumia mbinu katika kuchangamana kwako na wazazi au ndugu wa mtoto anayelelewa ili kujenga ushirikiano mzuri unaowezakana kati ya wanaohusika. Mtoto anayelelewa anapaswa kuona makubaliano na heshima ya pande mbili kati ya familia mlezi na wazazi, na mtoto hapaswi kuingizwa kwenye migogoro baina ya familia hizo mbili.

Tafadhali tumia dakika 15 (au muda mwingi kwa kadiri unavyohitajika) kwa ajili ya kuhitimisha ulichokifanyia kazi kati ya somo la mwisho na hili la sasa:

•  Je, ulifanikiwa kukamilisha kile ulichokipanga?
•  Nini kilikuwa rahisi kukifanya na kipi kilikuwa kigumu?
•  Je, ulijifunza nini kwa kufanya ulichokipanga?
•  Kipi utafanya vizuri zaidi wakati ujao katika masomo?

Tafadhali kumbuka: Haina shida kama ulipata matatizo-hii ndiyo namna mpya ya kufanya kazi, inahitaji kufanyia mazoezi kabla haujazoea.