Somo la 14/15

Ukurasa wa 2/7 Utangulizi wa Mada: Kuonyesha maarifa ya kitaalamu

Utangulizi wa Mada: Kuonyesha maarifa ya kitaalamu

KUNA MATARAJIO NA MAJUUMU GANI KWA MTOTO ANAYELELEWA ANAPOKUA KIJANA BALEHE?

Tafadhali tafakari maswali haya – una maarifa ya kitaalamu yenye thamani sana kutokana na maisha yako ya ujana:

  1. Ulipata uzoefu gani katika mabadiliko yako ya kutoka utotoni na kuwa kijana?
  2. Ni kwa vipi uhusiano wako wa kijamii na kundi rika ulibadilika?
  3. Ulipata uzoefu gani wa mabadiliko yako ya kimwili?
  4. Ulipata uzoefu gani wa mabadiliko yako ya kihisia?
  5. Ni kitu gani kilikufanya ukasirike au uone aibu?
  6. Ni kwa jinsi gani tabia, mwenendo na mitazamo dhidi ya wazazi wako vilibadilika?
  7. Nini ambacho wazazi wako na watu wazima wengine walifanya kukusaidia – nini walifanya ambacho hakikuwa cha msaada?
  8. Je, uliwahi kupata mitanziko kati ya kuwa mtiifu kwa wazazi wako na kutaka kuwa na maisha huru? Tafadhali eleza.
  9. Kama hitimisho: Nini kilikuwa changamoto kubwa kwako kama kijana?

Tafadhali andika mawazo hayo kama ujuzi na uzoefu wako binafsi katika kumsaidia kijana wako anayebalehe unayemlea.

Kwa ujumla umri wa ujana wa mtoto unayemlea ni kama ule wa vijana, lakini kutokana na historia ya maisha ya utotoni yasiyo salama, kipindi cha ujana kinaweza kuwa na changamoto kubwa na hisia zinazweza kuwa kali kuliko kawaida. Katika kipindi hicho Uhusiano wa karibu kunabadilishwa katika jambo linalohusu namna ya kuondoa ukaribu na kutenganishwa vinavyoweza kutokea katika namna nzuri ili kufikia utu uzima wa kujitegemea na elimu.

Watoto ambao wamepata unyanyasaji au kunyimwa haki kwa kiasi kikubwa walipokuwa wachanga mara nyingi huanza mapema balehe (hii huenda ni utaratibu wa kuishi), baadhi wanaanza kuanzia umri wa miaka 8-10.

Utafiti unaonyesha kwamba kupangiwa mahali pa kuishi katika familia walezi inaweza kuwa changamoto ya kihisia kama mtoto amekuwa na maisha magumu katika kuanza maisha. Huu ni umri ambao mapenzi na ukaribu vinaweza kuudhi, na katika matukio mengi migogoro inaweza kusababisha kuingiliwa kwa mahali pa kuishi: kunaweza kuwa na ugomvi mkubwa na mikwaruzano, kijana anaweza kutoroka, kujitenga, kukataa kuwasikiliza wazazi walezi au kufikiri pamoja nao n.k. Sehemu kubwa inategemea nguvu ya ukaribu ambao umejengwa kabla ya maisha ya ujana na wazazi walezi. Kama umemlea kijana kutoka utoto hadi balehe na uhusiano unakuwa mgumu sana kwake kukaa katika familia, unapaswa kulichukulia hilo kama kitu kinachotokea mara kwa mara katika ulezi.Vijana ambao wanakasirishwa sana na mapenzi kwa hakika mara nyingi wanakuwa na matatizo kidogo ya kushirikiana na walezi wataalamu ambao hawako karibu nao sana.

UKUAJI WA JUMLA NA MAJUKUMU WAKATI WA KUSHUGHULIKA NA VIJANA BALEHE

Katika balehe kijana pia inabidi abadilike na kujitegemea mwenyewe, na atabadilika kabisa kutoka utegemezi wa kitoto na imani, na kujaribu kupata uhuru kwa kuwa mbali na wazazi walezi. Mara nyingi kijana atahisi haja ya kuwatembelea wazazi waliomzaa na ndugu ili kujua uongo ni upi na ukweli ni upi.

Kujibainisha na kundi rika kunakuwa muhimu sana kuliko kujibainisha na wazazi walezi. Masuala kama “Ni lini nitakuwa nyumbani jioni – naweza kwenda kwenye hii tafrija – naweza kutoboa masikio yangu?” n.k. hujitokeza. Tafiti zinaonyesha kwamba vijana katika ulezi wana matatizo makubwa katika kufuata makundi rika: wazazi walezi mara nyingi wana hofu (na mara nyingi kwa nia nzuri) na kitakachotokea kama kwa mfano wakimruhusu kijana kwenda kwenye tafrija. Matokeo yake wanakuwa wakali zaidi kuliko wazazi wengine na hili linakuwa tatizo kubwa kwa kijana.

Hakuna suluhisho rahisi kwa matatizo hayo, bali baadhi ya mbinu za kiutaalamu ambazo zinaweza kusaidia.