Somo la 14/15

Ukurasa wa 1/7 Vijana na kuondoka mahali pa kulelewa

Vijana na kuondoka mahali pa kulelewa

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

•  Kuelewa changamoto za kawaida za kubalehe kwa vijana na familia mlezi.
•  Kumwandaa mtoto kwa ajili ya balehe kupitia mazungumzo
•  Kusimamia udhibiti wa mzazi mlezi dhidi ya uhuru: kuafikiana badala ya kudhibiti.
•  Umuhimu wa kundi rika.
  Mipango baada ya malezi.
  Sherehe ya “kuondoka nyumbani”.

Maudhui ya somo:

Katika mafunzo haya unakwenda kufanya na kusaidia awamu ya mpito wakati mtoto aliyeyelewa anakuwa kijana balehe na anaanza kujenga utambulisho wake mwenyewe. Pia utafanya kazi ya kumsaidia kijana mdogo wakati anaondoka kwenye familia mlezi.

 

Malengo ya somo:

Lengo la somo ni kupendekeza kwako namna ya kuelewa na kusimamia mabadiliko kwenye maisha ya familia mlezi wakati mtoto anapokuwa kijana na pia ni kwa vipi unaweza kusaidia kipindi mpito kutoka ulezi hadi kuishi kama mtu mzima.