Somo la 15/15

Ukurasa wa 5/5 Mpango kazi: Mambo tutakayofanya siku zijazo

Mpango kazi: Mambo tutakayofanya siku zijazo

Pendekezo la 1:

Kutokana na maelezo katika somo hili, tunapendekeza ufanye uwasilishaji mfupi wa ripoti uliyoandika kuhusu mafanikio na mazoezi ya kitaalamu katika ulezi wako. Hili linaweza kuchangia katika kutambuliwa na viongozi wako, watoa maamuzi na uhusiano wa utaalamu.

Tafadhali zingatia kwamba ripoti itasomwa na watu ambao hawaifahamu kazi yako.

Ielezee kwa maneno rahisi unachokifanya, unafanya kazi na nani, jinsi unavyotenda, na maadili ya binadamu unayofanyia kazi. Isiwe ndefu zaidi ya kurasa 3-5, na unaweza kuingiza picha kutokana na kazi yako ya kila siku kwa ufafanuzi. Kama umejaza fomu ya ujuzi, unaweza kuitumia kwa ajili ya ripoti.

Tafadhali amua nani ataandika ripoti (kwa mfano msimamizi, mwelekezi na wazazi walezi).

 

Pendekezo la 2:

Unaweza kutoa uwasilishaji wa video ya ulezi wako. Ionyeshwe katika matukio/mahojiano mafupi unachokifanya, unafanya kazi na nani, unatendaje, na unatumia maadili yapi ya kibinadamu. Isiwe ndefu zaidi ya dakika 10.

Kama inawezekana, unaweza kujumuisha mahojiano na mtoto wako unayemlea (kwa mfano: “Familia inayomlea Andrei”) na pengine jumuisha pia watu katika mtandao na wazazi waliomzaa.

Asante kwa utayari wako na kila la heri katika kazi yako hadi somo linalofuata!