Somo la 2/19

Ukurasa wa 3/4: Utangulizi wa Mada: Mada A na Mada B

Mada A: Ni kwa vipi maadili katika maisha ya familia yetu yanakuwa msingi wa kazi yetu kama familia mlezi?

Madhumuni ya zoezi hili ni kwamba wanafamilia wote wajihusishe katika mchakato wa kuwa familia mlezi. Familia mlezi inatoa maadili na matendo mazuri. Kama familia walezi, hamtarajiwi kuwa wataalamu, bali kutambua kile ambacho mko tayari kukitoa katika matunzo ya muda mrefu kwa mtoto anayelelewa: Maisha ya familia na matunzo ya kila siku. Zoezi hili litawasaidia wanafamilia wote kushirikishana na kujua maadili unayoweza kuyatoa kwa mtoto anayelelewa.

Kitu gani kinaifanya familia yako iwe muhimu:
Tafuta mchana mmoja au jioni ambapo wewe kama mzazi mlezi na watoto wako mwenyewe (kama unao) mnaweza kuzungumza kwa saa kadhaa bila ya kusumbuliwa. Zimeni simu zenu. Kama una rafiki mzuri wa familia au bibi au babu ambaye ni muhimu kwa familia yako, unaweza kuwaalika pia. Kama maswali ya kwanza yanachukua muda mrefu, labda unaweza kutumia mchana au jioni mara mbili.

Chukua karatasi na andika (Kama una watoto wako mwenyewe wanaweza kuchora).

  1. Shirikianeni pamoja kueleza siku moja katika maisha ya familia yako ambapo nyote mngesema kwamba hii ilikuwa ni siku nzuri ambayo haijawahi kutokea – siku ambayo mlishukuru na kupendana, kucheka sana na kufurahi. Au unaweza kuchagua siku ambapo nyote mliweza kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kusaidiana licha ya shughuli nyingi. Tafadhali alezaneni siku hii – mlifanya nini kilichoifanya siku hii iwe nzuri sana?
  2. Tafuta mambo matatu ambayo kila mwanafamilia anayathamini sana kuhusu maisha ya familia yenu. Kwa mfano: Tumekuwa na mazungumzo mazuri kwenye meza ya chakula, tunaweza kushirikiana kama ni lazima, au tunajivunia jinsi tulivyo. Andika maadili yenu ya msingi.
  3. Andika orodha kutokana na mlichokizungumzia: huo ni ujuzi wetu kama familia na kama familia mlezi.
  4. Mwambie kila mwanafamilia: Tutatumiaje ubora na ujuzi kutoa malezi mazuri kwa mtoto wa kulea tunayempokea au ambaye tumeshampokea?

Mada B: Kuandaa mtandao wako wa eneo: Bainisha watu wa kukusaidia

Andika orodha ya watu katika mtandao wako wa kijamii ambao wanaweza kukutana na mtoto au wanaweza kuwa muhimu kwake: Huyu anaweza kuwa muuza duka wa karibu yako, majirani na watoto wao, marafiki na ndugu, shule ya chekechea katika eneo au shule kama unapanga mtoto kutumia taasisi hizo.

Unapozungumza na watu katika mtandao huo unaweza kutumia tukio lolote la kijamii ili kuanzisha mada ya uamuzi wako wa kuwa kama familia mlezi. Huenda unakutana na watu unaowajua mtaani na kuzungumza kuhusu maisha yako ya kila siku.

Ni wazo zuri kuwa mkweli na muwazi tangu mwanzo kwamba umefanya uamuzi huo, na kwamba unafikiri hili ni jambo zuri kwa maendeleo ya familia yako, kwamba unatarajia kumtunza mtoto wa kulea. Unapaswa kuonyesha kwamba unafikiri mtoto aliye katika malezi sio aibu, bali malezi hayo kwa mtoto ambaye hana wazazi ni wajibu wa kawaida wa jamii.

Kama watu unaozungumza nao wana mashaka au chuki kuhusu watoto wa kulea, usianzishe mgogoro – wasikilize tu au sema kwamba unaelewa na kwamba hili linaweza kubadilika watakapokutana na mtoto.

ORODHA YA WATAALAMU KATIKA MTANDAO
Baada ya kuzungumza na majirani, marafiki na familia, wafikirie watu watatu ambao unadhani wana mitazamo chanya katika mazingira ya malezi yako.

Orodha inaweza kukusaidia kubainisha wataalamu wa siku zijazo katika mtandao wako wa kijamii, na unaweza kuzingatia katika kujenga uhusiano mzuri na watu wazuri.

Kama kuna watu wenye mitazamo hasi kuhusiana na ulezi au wenye chuki dhidi ya watoto wanaolelewa (“Unawezaje kukaa na mtoto ambaye hamna uhusiano?”). Jiulize namna unavyoweza kupunguza ushawishi wa watu hao, au unaweza kujitahidi kuwapa mtazamo mzuri zaidi kupitia matukioya kijamii ambako wanakutana na wewe na mtoto anayelelewa.