Somo la 2/15

Ukurasa wa 1/4: Kutoka familia ya mtoto hadi familia mlezii: Kupafanya nyumbani kwako kuwa mahali pako pa kazi

Kutoka familia ya mtoto hadi familia mlezi: Kupafanya nyumbani kwako kuwa mahali pako pa kazi

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

•  
Kupanga maadili mazuri katika familia mlezi.

•  Kujenga uelewa wa namna maadili hayo yalivyo nyenzo ya kuendeleza malezi ya kitaalamu.
  Kuwaandaa wanafamilia kwa ajili ya majukumu yao mapya.

Mada ya somo:

Katika somo hili la mafunzo utafanyia kazi mchakato wa kuwa mtaalamu wa sehemu ya matunzo na kutafuta ujuzi wa kitaalamu wa maisha ya familia yako.

Malengo ya somo:

Lengo kuu la somo hili ni kupanga maadili ya familia ambayo yatakuwa ujuzi wako wa kitaalamu katika kazi ya kuwa familia mlezi.

Tafadhali tumia dakika 15 (au muda mwingi kwa kadiri unavyohitajika) kwa ajili ya kuhitimisha ulichokifanyia kazi kati ya somo la mwisho na hili la sasa:

•  Je, ulifanikiwa kukamilisha kile ulichokipanga?
•  Nini kilikuwa rahisi kukifanya na kipi kilikuwa kigumu?
•  Je, ulijifunza nini kwa kufanya ulichokipanga?
•  Kipi utafanya vizuri zaidi wakati ujao katika masomo?

Tafadhali kumbuka: Haina shida kama ulipata matatizo-hii ndiyo namna mpya ya kufanya kazi, inahitaji kufanyia mazoezi kabla haujazoea.