Somo la 3/21

Ukurasa wa 2/6: Mtoto anahisi vipi anapoanza kuishi katika ulezi? Kuelewa kipindi cha mpito

Mtoto anahisi vipi anapoanza kuishi katika ulezi? Kuelewa kipindi cha mpito

Mtoto anapowasili katika familia mlezi uliyoiandaa kwa ajili ya kukutana, na huenda utatarajia kutumia ujuzi wako wote kumsaidia mtoto kuzoea katika familia mpya.

Ni muhimu kugundua kwamba kuwasili kwenye familia mlezi ni vigumu zaidi kwa mtoto kuliko kwa familia mlezi: huenda kumekuwa na matukio ya fujo na kuchanganyikiwa, hususan kama mtoto amechukuliwa kutoka kwa wazazi kinyume na matakwa yake. Hata kama mtoto ameandaliwa vizuri, kuwekwa mahali ni uzoefu mgumu sana kwa watoto, na anahitaji muda wa kutosha kuzoea kabla ya kuanza kujisikia ana ulinzi katika familia mlezi.

HALI YA UKINZANI: KUPOTEZA FAMILIA YAKO NA KUKUTANA NA WENGINE WAKATI HUOHUO
Hii ni hadithi ya kweli kutoka kwa mtoto mwenye umri wa miaka kumi anayelelewa kuhusu namna alivyohisi katika mwaka wa kwanza wa malezi. Wakati huo alikuwa na miaka sita.

Kwa hakika sikuwapenda (familia mlezi) pamoja na kwamba walikuwa wakarimu kwangu, kwa sababu tu walikuwa wageni. Nilimkumbuka mama yangu na rafiki zangu wakati wote, kila wakati wazazi wangu walezi waliponitendea vizuri ilinifanya nimfikirie mama yangu. Nilifikiri lazima niwe mtoto mbaya kwa kuwa walinichukua. Chumba kilikuwa kipya na nyumba yao ilikuwa na harufu tofauti ambayo sikuipenda. Niliogopa sana mwanzoni na nililia sana wakati walipokuwa hawanioni, na mara moja nilijaribu hata kutoroka, lakini sikuweza kupata basi sahihi, hivyo nilirudi pale. Waliponipa kitu nilihisi Mama yangu asingeweza kumudu hilo na ndiyo sababu walinichukua, hivyo niliwafokea kwamba walilipwa ili wanilee na kwamba hawakunipenda kabisa. Iliwafanya wawe na huzuni sana, lakini nilikuwa na hasira sana kwa kuondolewa kwetu. Niliogopa kuwa kama ningewapenda, mama yangu angenikasirikia. Nilifikiri rafiki zangu na Mama yangu wamenisahau kabisa, hivyo nilifurahi sana wakati (wazazi walezi) waliponirejesha nyumbani kwetu na kunisaidia kuandika barua kwa rafiki zangu. Sasa najua kwamba kwa kweli walinipenda, na wakati mwingine tulizungumza namna nilivyokuwa na tabia mbaya nilipoanza kuishi hapa, na tulicheka kuhusiana na hilo…”

Hadithi hii inaonyesha jinsi mtoto anayeanza maisha ya kulelewa anavyokuwa katika hali ya kushtuka, huzuni na kuchanganyikiwa wakati akijaribu kujiweka katika mazingira mapya.

Hakika mtoto yuko kwenye hali ya ukinzani wenye mgogoro – anakuwa amepoteza watu muhimu, na katikati ya upotezaji huo ni lazima akubaliane na watu wanaotaka kuwa wazazi wake na kuwa karibu naye.

Katika masomo yanayofuata (“Kutoka katika hali ya uchungu na kurejea katika hali ya Kawaida” na “Mimi ni nani?”), utajifunza mengi zaidi kuhusu uhusiano wa karibu na jinsi watoto wanavyoonyesha hisia kwa kuondokana na familia zao. Mada zinazofuata katika somo hili zitakuandaa kwa namna ya kukubaliana kuanzia kwenye hisia za mwanzo za mtoto wakati wa mpito kutoka kwa walezi wa awali hadi ulezi wako.

Angalia video hii ya Saleh, ambaye amekulia kwenye SOS Children’s Village ndani ya Tanzania. Anaelezea uzoefu wake jinsi anavyokumbuka familia yake na jinsi anavyopata usalama pamoja na mama yake wa SOS, ambaye anaweza kuongeanaye kila jambo ambalo anafikiria katika kicha chake.