Somo la 3/21

Ukurasa wa 3/6: Mada ya Utangulizi: Mada A na Mada B

Mada A: Udhibiti na subira katika kipindi cha mpito

Walezi wana tabia ya kutozingatia ni muda gani inamchukua mtoto kutulia katika mazingira mapya na kuanza mchakato wa uhusiano wa kihisia na wazazi walezi. Unapaswa kufikiria mwaka wa kwanza kama kipindi cha mpito ambapo mtoto anatumia nguvu zake zote kujiweka sawa katika mazingira yake mapya. Kama mtoto ni mkubwa inaweza kuchukua muda mrefu. Mtoto lazima apange upya hisia zake zote na mawazo, na hili linahitajika sana.

Kama wazazi walezi wana wasiwasi kwamba sio wazuri kiasi cha kutosha na kutaka kuonyesha hilo, wanaweza kuangalia tu katika maendeleo ya mtoto na kuweka mahitaji mengi sana kwa mtoto kwa ajili ya tabia nzuri, kutarajia dalili za upendo na maendeleo ya haraka katika ukuaji. Ni vizuri kufikiria kipindi cha kwanza kama kipindi cha kuridhika: mtoto anahitaji kupumzika, kubembelezwa, kuliwazwa na uvumilivu. Anapita katika matatizo.

Kama wazazi walezi mnaweza kumsaidia mtoto kwa kudhibiti hisia zake – mtoto anaweza kuwa na msongo mkubwa muda wote, au hasira sana au kuwa na huzuni. Uitikiaji wako uwe wa utulivu na ukarimu na usichukulie hisia hizo binafsi – ni za kawaida katika mazingira mapya na magumu. Pia unapaswa kuwa mvumilivu sana na usihitaji mambo mengi au matarajio kutoka kwa mtoto. Jambo muhimu sana ni kumsaidia mtoto kuwazoea walezi wapya na mazingira mapya na hupaswi kuzingatia sana katika kumfundisha mtoto ujuzi mwingi katika kipindi cha mpito.

Mada B: Epuka kutengana na mtoto na tengeneza taratibu salama za kila siku

Ni wazo zuri kutotengana kimwili na mtoto kwa miezi michache ya kwanza – mmoja kati ya wazazi walezi anapaswa kuwepo wakati wote na unapaswa kumfikiria mtoto kama mtoto anayehitaji kuliwazwa na kuwepo kwa walezi kama ambavyo mtoto mdogo angefanya. Wazazi wengi walezi wanaweza kueleza kuhusu watoto wao wanaowalea wanapoingiwa na hofu kwa sababu ya kuachwa peke yao kwa mud. Hali hii itakwisha baada ya muda fulani – wakati mwingine ni muda mrefu zaidi kuliko ulivyofikiria awali, hivyo uwe mvumilivu sana.

Sio wazo zuri kufanya shughuli nyingi, safari za mapumziko na kuwaalika marafiki au familia mwanzoni – hii itasababisha ugumu zaidi kwa mtoto kuzoea mazingira. Jaribu kuwa na siku nyingi ambazo mtakuwa pamoja na wewe kwa muda mrefu na kufanya vitu vya kila siku pamoja, kabla ya kuwashirikisha wengine.

Katika kipindi cha mpito mtoto anahitaji kujifunza utaratibu wa kila siku katika familia. Hii ni njia inayosaidia sana kumuondoa mtoto katika hali ya vurugu: Rudia jambo lilelile kila siku na wakati uleule! Kwa mfano, kusoma hadithi hiyo hiyo ya wakati wa kulala mara nyingi inaweza kuwa njia nzuri ya kuonyesha kwamba nyumba yako inatoa eneo imara la kuishi. Kwa watoto wakubwa, kufanya kazi na shughuli hizo hizo kila siku kunaweza kuwa na utulivu. Fikiria desturi na shughuli ndogndogo unazoweza kufanya katika maisha ya kila siku ili kuunda dunia inayotabirika kwa mtoto.