Somo la 3/15

Ukurasa wa 1/6: Kumpokea mtoto wa kulea

Kumpokea mtoto wa kulea

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

•  Kujenga utambuzi kuhusu namna watoto wanavyokuwa na hisia ya mabadiliko ya walezi.
  Kumsaidia mtoto kujisikia salama katika familia yako mlezi.

Mada ya somo:

Katika somo hili la mafunzo utatambulishwa namna watoto wanavyoweza kujisikia kwa familia mpya na mazingira, na namna unavyoweza kumsaidia mtoto kujisikia salama katika mazingira mapya, familia yako mlezi.

 

Malengo ya somo:
Malengo ya somo ni kukupa uelewa wa namna watoto wanavyoitikia mazingira mapya, na kukupa mapendekezo ya kuendana na kipindi cha kwanza cha kupangiwa mahali pa kuishi.

Tafadhali tumia dakika 15 (au muda mwingi kwa kadiri unavyohitajika) kwa ajili ya kuhitimisha ulichokifanyia kazi kati ya somo la mwisho na hili la sasa:

•  Je, ulifanikiwa kukamilisha kile ulichokipanga?
•  Nini kilikuwa rahisi kukifanya na kipi kilikuwa kigumu?
•  Je, ulijifunza nini kwa kufanya ulichokipanga?
•  Kipi utafanya vizuri zaidi wakati ujao katika masomo?

Tafadhali kumbuka: Haina shida kama ulipata matatizo-hii ndiyo namna mpya ya kufanya kazi, inahitaji kufanyia mazoezi kabla haujazoea.