Somo la 4/19

Ukurasa wa 4/5: Msingi Usalama na Ugunduzi: Kucheza na kushirikiana na wengine

Msingi Usalama na Ugunduzi: Kucheza na kushirikiana na wengine

Kama mtoto anajifunza kutengana bila kuwa na hofu kubwa, umempa Msingi Usalama. Mtoto mwenye msingi usalama hajichoshi mwenyewe na hofu ya kuachwa, kulia na kung’angania, anajisikia salama. Hivyo, unapotembea na watoto, unapaswa wakati wote uanze kwa kuwepo na sio kuondoka kila wakati. Kama utakaa mahali ambapo upo karibu na mtoto, mtoto atakuwa mtulivu na hatakuwa na hofu kuwa unaondoka.

Kama utampa mtoto msingi usalama, mfumo mwingine wa tabia unaweza kuendelea: Mfumo wa Kugundua. Hivyo “Unaondoa” Mfumo wa Uhusiano wa karibu kwa kuwa mtulivu na kuwasilisha, na kisha “unaanzisha” moja kwa moja Mfumo wa Kugundua.

Mtoto aliye salama pamoja na mlezi ambaye anakaa mahali alipo ataanza kukaa mbali na yeye, kuchezea vitu, kujifunza, kuangalia dunia, kutaka kujua mambo, kukutana na watoto wengine na kufanya majaribio kadhaa.

Hii inaitwa tabia ya ugunduzi, na ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto. Watoto wenye afya wanang’ang’ania tu kuwa na walezi kwa muda mfupi hadi watakapojihisi wako salama. Kisha wanaanza kucheza, kuchunguza, n.k. Hii ni njia pekee wanayoweza kujifunza kuhusu dunia na kuhamasishwa kwa kufundisha na kujifunza baadaye katika maisha. Hivyo, watoto salama wanajifunza zaidi kuliko watoto wasiokuwa salama ambao wanatumia nguvu zao kujaribu kuepuka kutengana.

Kwa mfano, unampeleka mtoto katika kundi jingine la watoto. Mwanzoni, atakung’ang’ania miguu yako na kulia (tabia ya uhusiano wa karibu) lakini kama utaendelea kuwepo katika eneo lilelile na kuwa mtulivu, mtoto atatambaa kutoka kwako kuelekea sehemu nyingine, kuchezea midoli, na kukutana na watoto wengine (tabia ya ugunduzi). Kama ukisimama na kuondoka mtoto ataacha kuchunguza na kurudi na kukung’ang’ania tena ili kukuzuia usiondoke (tabia ya kuwa karibu).

MASWALI
  • Unaweza kukumbuka kuwaona watoto wakikung’ang’ania na kulia wakati unaondoka?
  • Je unajaribuje kufanya utenganishaji – kumuacha mtoto au kumhudumia mtoto mwingine?
  • Unakaaje na watoto na kuwapa “Msingi Salama” katika kazi yako?
  • Ni wakati gani unapomuona mtoto anajisikia kuwa salama akitambaa kuelekea mbali na wewe na kuanza kucheza na watoto wengine au kuchezea vitu na midoli?
  • Utafanyaje mchezo wa “peek-a-boo” na “mchezo wa kujificha” katika kazi zako za kila siku?
  • Je, kuna watoto ambao hawachunguzi na kucheza, lakini wanakung’ang’ania wewe wakati wote? Unawafanyaje wajisikie wako salama zaidi?

Hapa kuna mifano miwili ya mama anayetengeneza secure base kwa kikundi cha watoto. Mfano wa kwanza, mama anatengeneza mpango wa chakula pamoja na watoto. Mfano wa pili, katika shughuli ya pamoja, mama anauliza kila mtoto kuhusu shughuli zake za shule. Vitu vya msingi ni kushirikisha, malengo, na uwepo wao.

Mfano wa secure base na exploration: Hapa unaona mama anayetengeneza secure base kwa mtoto wake. Mbeleni ya video utaona jinsi mtoto anavyojisikia salama mpaka anaweza kutembea kutoka kwa mama na kuanza kucheza na mpira wake peke yake. Huu ni mfano bora wa exploration.

MASWALI
  • Ni jambo gani ambalo mama wa kituo hiki cha matunzo ya watoto anafanya ili kumfanya mtoto ajisikie salama?
  • Kwa nini aina hii ya utendaji (kukaa sakafuni, kusimama muda mwingi) kunawafanya watoto kuchunguza na kujaribu kupata mpira? 
  • Unafanyaje watoto wanapolia kwa sababu tunaondoka?
  • Unakereka au unavumilia?
  • Je, watoto wanakuona wakati mwingi wanapokuwa macho?
  • Kuna ugumu gani unapojaribu kukaa na watoto wakati mwingi?
ORODHA YA MAMBO YA KUELEWA
  • Utaitambuaje tabia ya kuwa karibu?
  • Jambo gani ambalo mlezi anafanya kumpa mtoto msingi usalama?
  • Unawafundishaje watoto kutengana bila kuwa na hofu kubwa?
  • Unawezaje kutambua tabia ya ugunduzi?
  • Kwa nini tabia ya gunduzi ni muhimu sana kwa ukuaji mtoto?
MAPENDEKEZO YA ZOEZI
  • Tazama video ya “Msingi Salama” wa mama anayewaangalia watoto kwa kutwa. Tazama jinsi anavyokaa katika eneo moja sakafuni na kujenga msingi salama. Watoto wanaanza kuchunguza kwa sababu hazunguki sana. Tafakari jinsi utakavyotoa msingi salama kwa watoto kupitia kazi zako.
  • Tafakari kuhusu kazi zako za kila siku: Baada ya kuelewa umuhimu wa uhusiano wa karibu na ugunduzi, kuna uboreshaji wowote unaotaka kuufanya katika utendaji wako wa kila siku pamoja na watoto?
  • Kama ndivyo, unaweza kuweka mpango – utafanya nini tofauti, utaanza lini, utajuaje kwamba umepata matokeo unayoyataka? Unaweza kutumia kamera kwa ajili ya kurekodi utendaji wetu kabla na baada ya kufanya mabadiliko?