Somo la 4/15

Ukurasa la 5/5: Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Mpangokazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

  • • A. Fuatilia na kumbuka, au rekodi video fupi ya watoto wachanga au watoto ambao wanaonyesha hisia na tabia ya uhusiano wa karibu wakati mlezi anapoondoka.
  • B. Rekodi video ndogo ya mlezi anayejaribu kuwa msingi salama.
  • C. Rekodi namna watoto tofauti wanavyoonyesha hisia kwa walezi wao wanapoondoka (wanavyomng’ang’ania mlezi au kuanza kumtafuta, kutambaa kuelekea mbali na yeye n.k.).
  1. Kama ulitumia simu yako ya mkononi: Utahakikishaje kwamba ni wewe tu, walezi wengine na mwalimu wanaangalia kilichorekodiwa?
  2. Mnatunzaje kilichorekodiwa kwa usalama ili kukitazama baadaye (mfano katika kompyuta kwa kutumia msimbo wa kutazamia)?
  3. Baada ya kutunza vyote vilivyorekodiwa katika kompyuta moja, hakikisha vimefutwa katika simu za mkononi au kamera ulizotumia kurekodia.

Asante kwa utayari wako na kila la heri katika kazi yako hadi somo linalofuata!