Somo la 5/19

Ukurasa wa 2/5 Mada A: Kwa nini uchocheaji wa hisia kimwili ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa ubongo na uhusiano wa karibu?

Mada A: Kwa nini uchocheaji wa hisia kimwili ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa ubongo na uhusiano wa karibu?

Kwa mamilioni ya miaka, mamalia wamekuwa wakifanya ugusanaji wa mwili kati ya mama na mtoto. Utawaona mbwa; paka, ng’ombe au mamalia mwingine yeyote wakiwalamba watoto wao mara nyingi baada ya kuwazaa na kuwagusa kwa karibu katika miili yao kwa kulala karibu nao. Hii sio kuwafanya tu kuwa wasafi bali kulamba pia “huamsha” ubongo wa mtoto na kuufanya uchangamke na kugusana miili ni “chanzo” muhimu cha uhusiano wa karibu na kuunganisha hisia kati ya mtoto na “mama”. Mtoto ambaye hatalambwa baada ya kuzaliwa anaweza kufa baada ya muda mfupi kwa sababu ya kukosa uchangamfu wa ubongo. ”Msongo mkubwa wa mawazo” kimsingi unamaanisha “utendaji mdogo“, hivyo msongo wa mtoto huanzia katika ukosefu wa uchocheaji wa hisia za mwili, kusababisha kiwango kidogo cha utendaji kazi wa ubongo. Watoto waliowekwa mahali au kutelekezwa wanakabiliwa na kukosa uchocheaji huu, kwa kuwapoteza walezi wao wa kwanza au kuwa katika taasisi ambazo hazina walezi wa kutosha. Wazazi wengi wenye matatizo ya miili yao kutofanyakazi vizuri hawana uwezo wa kuwachangamsha watoto wao kimwili, na watoto wengi hawajachangamshwa kiasi cha kutosha kabla ya kufika katika taasisi au katika familia mlezi.

Binadamu wanazaliwa na akili ambayo haijakomaa na isiyo tengemaa, na mwanzo wa maisha, shughuli ya akili inaweza kuongezeka tu na kutengemaa kama mtoto anachochewa mara kwa mara na kuguswa mwili.

Ugusaji (kugusana ngozi) baada ya kuzaliwa ni muhimu sana pia kwa “kuanza” mfumo wa uhusiano wa karibu
Matatizo katika ukaribu wa mapema huonekana kama mama wa mtoto aliyezaliwa amezuiliwa dhidi ya ugusaji na kumchukua mtoto wake aliyezaliwa kila wanapohisi umuhimu wa kufanya hivyo

Kwa mfano katika utafiti wa hospitali kuhusu kujifungua: Pale mtoto mchanga anapoondolewa kwa mama yake kulingana na ratiba ya siku iliyopangwa, mama atakuwa akijisikia kuwa na hatia mara kwa mara, kuwa na wasiwasi zaidi katika kuelewa na kutafsiri jinsi mtoto anavyojisikia na anahitaji nini na kutokuwa salama zaidi katika kuchukua uamuzi kuhusu utunzaji wa mtoto.
Kama kipindi cha kutengenishwa kimwili kitakuwa kirefu sana, mama anaweza kupoteza hisia za kuwa karibu na mtoto wake na kumchukulia kama mgeni. Hisia za kuungana zinategemeana na uhuru wa kugusana mwili kwa mama na mtoto kwa muda mrefu baada ya kuzaliwa
 Kuzaliwa kabla ya muda wake na matatizo wakati wa kuzaliwa sio tu matatizo ya hali ya kimwili ya mtoto, mtoto mchanga aliyezaliwa atakuwa akitenganishwa na mama yake mara kwa mara kwa sababu za kitabibu (chombo cha kukuzia watoto njiti), na hili linaweza kuwa na matokea mabaya katika utendaji wa ubongo wa mtoto na hisia za mama kutokuwa karibu na mtoto. Kwa sababu hii katika vitengo vingi vya watoto baada ya kuzaliwa, akina mama hawatenganishwi tena na watoto wao wachanga.

Unaweza kupata video nyingi katika YouTube kwa mfano kuonyesha mbinu za kumsinga mtoto.

Mfano wa mbinu za kumsinga mtoto.

MBINU ZETU ZA KUWACHANGAMSHA WATOTO HATA KAMA AKINAMAMA WANAFANYA KAZI– “KUNYONYESHA KWA MUDA MREFU”
Wakati makabila ya binadamu yalipoanza kuzunguka, ilibidi tutafute njia nyingine ya kuwachangamsha na kuwalisha watoto.

Hivyo, wanawake wana maziwa mawili tu juu mbele ya kifua, na wenyeji huwabeba watoto wao mikononi. Hii inawezekana ndiyo sababu binadamu walikuwa na uwezo wa kusambaa dunia nzima: Hata mama mwenye mtoto mchanga aliyezaliwa anaweza kutembea kwa umbali mkubwa na hivyo makundi ya binadamu walikuwa na uwezo wa kuhama kutoka kambi moja hadi nyingine. Pia watoto wa binadamu wana vichwa vikubwa wakati wa kuzaliwa, hivyo kama walivyo kangaruu tunatakiwa kuzaa kabla ubongo wa mtoto haujawa tayari kufanya kazi wenyewe.

Unaweza kusema kwamba kwa miezi nane ya kwanza baada ya kuzaa, tunazungumzia kuhusu “ kumalizia ujauzito nje ya tumbo la uzazi” – ni katika miezi tisa au kumi na mbili baada ya kuzaliwa mtoto anakamilisha utendaji thabiti wa ubongo.

MAJADILIANO YA KIKUNDI
Dakika 10
Tafadhali angalia picha na video na kisha jadili:

  • Je, wazazi wako na wazazi wa wazazi wako wanawachangamshaje watoto? Je, wanawabeba mwilini?
  • Je, wanatumia nyenzo yoyote ya uchangamshaji unayoweza kuiona –vitanda vidogo vya watoto, hamoki, n.k?
  • Kama unao au ulikuwa na watoto, ulishawahi kutumia mojawapo kati ya nyenzo hizo?
  • Watazame watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja katika utaalamu wako wa malezi:
    • Je, unawabeba mara nyingi mwilini?
    • Wanalala wapi?
  • Ni muda gani katika saa zao za kazi wanatumia kulala au katika kitu ambacho hakitingishiki au hakisogei? (Kama vile kitanda, sanduku au tenga ambamo mtoto huachwa na kucheza, au katika kigari cha kumwendeshea mtoto ambacho hakisogei)