Somo la 5/21

Ukurasa wa 3/5 Kwa nini kitanda si zana nzuri kwa utendaji kazi wa ubongo wa mtoto?

Kwa nini kitanda si zana nzuri kwa utendaji wa ubongo wa mtoto?

Vitanda vinafaa tu kulala kwa vipindi vya muda mfupi. Kubakia kitandani kwa muda mrefu hakuchangamshi.

Ni kweli kwamba utendaji kazi wa ubongo unapungua mtoto anapokuwa amelala kitandani.

Hupaswi kumwacha mtoto kitandani ukiwa unafanya kazi kwa muda mrefu, kwani mtoto hawezi kuchangamka akiwa amelala. Kinyume chake, ni kwamba ubongo wa mtoto utachangamka ukiwa umembeba.

Kama utamwacha mtoto katika kitanda kidogo kilichofungwa, mtoto atakuwa haoni vizuri na anazuiwa kuona shughuli za kibinadamu na kushindwa kujifunza kutokana na shughuli hizo zinazoendelea karibu naye.

Katika kitanda kidogo cha mtoto au hususani katika hamoku kama hilo lililo katika picha hii, mtoto anabembea kwa furaha, anahamasishwa na nguo, anaweza kujifunza kitu kinachoendelea karibu naye, na hawezi kukisahau.

KICHOCHEO CHA MWILI KINAREKEBISHAJE UTENDAJI KAZI WA UBONGO? MGUSANO WA NGOZI NA UCHOCHEAJI WENYE UWIANO
Tafiti zimeonyesha kwamba aina mbili za uchocheaji ni muhimu sana katika kuongeza utendaji kazi wa msingi wa ubongo.

Uchocheaji wa ngozi:
Ulimi na mdomo. Kwa mfano mtoto anaponyonya, au akiwa amelala kwenye mikono ya mlezi, au akiwa ananing’inia kweye mbeleko, au akiwa amefunikwa na kitambaa kinachofyonza maji kama taulo ambacho kinatoa kichocheo zaidi ya shuka. Watoto wachanga na watoto wanaojifunza kutembea hutafuta mgusano wa ngozi kwa kujaribu kupata mgusano huo kutoka kwa walezi.

Uchocheaji wenye uwiano:
(Kubembea, kuusimamisha, kuanza kuutikisa mwili). Kwa mfano mlezi anapombeba mtoto, wakati kitanda kidogo au hamoku inapotoka upande mmoja kwenda mwingine, wakati mlezi “anapomrusha mtoto hewani” na kumfanya acheke. Watoto wanaojifunza kutembea hutafuta uchocheaji mlingano kwa kujigeuza huku na kule na kupata kizunguzungu, na kwa kufurahia chombo kinachopita kwenye miinuko na miinamo mikali, kuning’inia upande mmoja hadi mwingine, bembea ya kuzunguka na shughuli nyingine za uchocheaji wenye uwiano.

Baadhi ya mifano kutoka katika tafiti mbalimbali za vichanga wanaozaliwa kabla ya muda na wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo:

  • Katika chombo cha kukuzia watoto njiti hakuna mjongeo na kuna kichocheo kidogo cha ngozi. Kama vichanga vikilazwa kwenye ngozi ya kondoo isiyo wa vijidudu vya maambukizo badala ya shuka laini, wataongezeka uzito wa gramu 15 zaidi kwa siku kwa sababu ya uchocheaji kutoka kwenye ngozi ya kondoo unaoongeza utendaji kazi wa ubongo –hivyo kusaidia umeng’enyaji mzuri wa chakula.
  • Kama unagusa na kupapasa polepole na ncha ya kidole sehemu ya nyuma ya vichwa vya watoto walio katika vyombo vya kukuzia watoto njiti kwa dakika mbili mara moja kwa saa, watatoa 20% zaidi ya asidi ya tumbo, hivyo ikiongeza hamu yao ya kula na kuongezeka uzito.
  • Katika nchi ambako chombo cha kukuzia watoto njiti na matibabu hayapatikani, watoto njiti wana kiwango kikubwa sana cha kuishi iwapo “Njia ya Kangaruu” inatumiwa –mtoto anabebwa na mlezi kwa siku nzima. Unaweza kujifunza njia hii zaidi hapa baada ya somo hili:

Tafiti nyingine zinaonyesha kwamba mapigo ya msingi ya mwili polepole yanaimarika wakati mtoto anapoguswa au kubembelezwa mara nyingi na walezi: Mapigo ya moyo, upumuaji, hamu ya kula, umeng’enyaji chakula, muda wa kulala, umakini, kutazamana ana kwa ana na uzingativu.

Kama utajifunza kuhusu mama huyu, utaona ni mara ngapi anatumia mguso na kubembeleza, na namna hili linavyofanya mtoto kutoa mwitikio na kuwa mchangamfu.

KUCHOCHEA WATOTO DHAIFU NA WANAOJIFUNZA KUTEMBEA WALIOCHOCHEWA KIDOGO

Watoto wachanga na wale wanaojifunza kutembea ambao walichochewa kidogo, na watoto njiti wana hisia zaidi kuliko ukawaida wa uchocheaji na kwa sababu hii wanajaribu kuepeuka uchocheaji. Kadri mtoto mdogo au mtoto anayejifunza kutembea anavyokuwa na hisia ndivyo unavyopaswa:

  • Kumchochea kwa taratibu sana (kwa mfano, mtoto kulala kwenye mikono yako pasipo kuitikisa sana au kuzungumza kwa sauti kubwa. Au mbembeleze mtoto kwa taratibu sana kwa sekunde chache, angalia anavyoitikia na fanya tena kwa dakika chache baadaye).
  • Anza kwa kumchochea mara kwa mara kwa vipindi vifupi sana, na taratibu mchochee zaidi kwa vipindi virefu (kwa mfano kubembeleza mtoto kwa sekunde chache na kurudia hili baada ya dakika chache, kisha siku hadi siku ongeza muda wa ubembelezaji na mguse zaidi)
  • Kuwa makini na ishara za uchocheaji uliozidi. Mtoto anaweza kushtuka, kujaribu kugeuza uso au kuanza kulia. Baada ya uchocheaji, mtoto anahitaji kupumzika kwa muda kidogo. Jaribu kutafuta chanzo cha uchocheaji wa mtoto na mapigo mazuri ya uchocheaji wa mtoto. Utaratibu huu unatofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine.

 

Watoto wanaosumbuliwa na athari za mama zao kunywa pombe wakati wa ujauzito (Athari za Pombe kwa Kijusi (FAE)), au mbaya zaidi ya (Dalili mbalimbali za athari ya Pombe kwa Kijusi (FAS)) wana hisia zaidi na chumba chao hakitakiwi kuwa na mwanga mkali, watu wanapaswa kutembea taratibu na kuzungumza polepole na kukaa kwa utulivu wakiwa wamewapakata.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu uchocheaji katika www.nofas.org/living/strategy.aspx
FAE na FAS mara nyingi husababisha matatizo ya muda mrefu katika maisha.

Pombe na dawa za kulevya:
 Dalili za kawaida za watoto waliothiriwa na dawa ni kufanya mambo yasiyo ya kawaida, hawali vizuri, mapigo ya haraka ya moyo, mjongeo usio wa kawaida na ulalaji usioridhisha. 
 Sifa nyingine ni kuzaliwa na uzito mdogo, low Agpa score (kipimo cha kupimia afya ya jumla ya mtoto, ikiwemo mapigo ya moyo na matendo yasiyo ya hiari yanayotokana na uchochezi wa neva) na mzunguko mdogo wa kichwa usio wa kawaida. Hata hivyo, dalili hizi mara nyingi husababishwa na mateso ya jumla ya mama, na kama atawekwa kwa mlezi wa kawaida baada ya kuzaliwa, mengi ya matatizo haya yatakwisha. 
 Kwa hiyo, kuwekwa katika taasisi au kwa familia mlezi ni muhimu sana mara tu baada ya kuzaliwa.

Kwa watoto wanaosumbuliwa na shambulio la kifafa uchocheaji unapaswa kupangwa pamoja na msaidizi wa kitabibu kama inawezekana. Mashambulio ya kifafa kwa watoto yanaweza kuchochewa na uchocheaji wa harakaharaka sana na mkubwa.

MAJADILIANO YA KIKUNDI

Dakika 10

  • Kwa nini ni muhimu watoto wanapobebwa kugusishwa na mwili wa walezi?
  • Ni vifaa gani vinavyotumiwa katika utamaduni wako kumchangamsha mtoto wakati mama yake anapokuwa na kazi nyingi?
  • Kwa nini kumlaza kitandani kupungue kuwa kwa vipindi vifupi vya kawaida vya kulala mchana?
  • Ni aina gani za uchocheaji unaonekana kufaa sana kwa utendaji kazi wa ubongo wa watoto?
  • Unapaswa kuwa makini na nini wakati wa kuwachochea watoto?