Somo la 6/19

Ukurasa wa 2/4 Mada A: Kazi na ufanyaji kazi kwa kujenga uhusiano

Mada A: Kazi na ufanyaji kazi kwa kujenga uhusiano

Watoto hawana budi kujifunza kutoka kwako jinsi ya kuwa karibu na mlezi, kujisikia kuwa na uhusiano wa karibu nao, jinsi ya kufanya vitu na jinsi ya kuchangamana na wengine. 
 Wanajifunza kutokana na namna unavyomudu ufanyaji kazi na kujenga uhusiano ili kuwa mtu unayechangamana kijamii.

Kwa maana hiyo, wewe kama mlezi, ni mtu muhimu sana katika maisha ya mtoto aliyewekwa mbali na familia yake.

Hawana wazazi wao kama walimu, hivyo ni lazima wawategemee walezi wao katika kujifunza. Kile walichotakiwa kujifunza kutoka kwa wazazi wao, sasa ni lazima wajifunze kutoka kwako. Wakati mwingine huu ni mzigo wa majukumu, lakini pia ni zawadi: Unapofanikiwa, unakuwa umeshampa mtoto msingi salama: msingi mzuri wa maisha.

Kulifanya jambo hili kwa vitendo si rahisi kama unawajibika kutoa huduma kwa watoto wengi, basi tuangalie kazi yenyewe:

  • Unapofanya kazi na watoto, wakati wote unafanya kazi mbili tofauti. Unafanya vitu vingi kwa vitendo: Kufanya shughuli na watoto, kuwavisha nguo, kuwalaza kitandani, kuwaogesha, kuwabadilisha nepi, n.k. Hii ni muhimu kwa ajili ya kutekeleza mahitaji ya mtoto (chakula, kulala, shughuli) na kufanya midundo asili ya shughuli wakati wa mchana.
  • Wakati unapofanya yote haya, pia unafanya kazi ya kujenga uhusiano: wakati unamvalisha nguo, pia unaongea na mtoto, unamjibu mtoto, unapata uzingativu wa mtoto, unatabasamu na kumpapasa mtoto na kadhalika. Hii ni lazima ili kumfanya mtoto ajisikie salama, kwa ajili ya kuendeleza ukaribu, na kwa ajili ya elimu ya kijamii na kihisia kwa ujumla.

Angalia video hii na kufikiri jinsi unavyoweza kuhusiana na watoto wakati unafanya kazi ya mkono kwa wakati moja.

MASWALI
  • Ni nini cha muhimu zaidi au cha lazima kwako – ni kwa namna gani unawianisha kazi na kujenga uhusiano katika huduma yako ya malezi.
  • Ni kwa vipi unawianisha kazi na uhusiano katika familia yako mwenyewe? Wazazi wako walilifanyaje jambo hili?
  • Kwa nini una uwianisho ulio nao katika huduma yako ya malezi – Je, hii ni kwa sababu “Ninafanya hivi mara zote”, “Nina kazi nyingi”?
  • Yapi ni matatizo ya kila siku katika kuwianisha kazi na kujenga uhusiano kazini kwa upande wako?
  • Je, unawishanishaje kati ya ” kutoa muda na uzingativu kwa mtoto mmoja” na kutoa uzingativu kwa watoto wote’? Unapokuwa na watoto wengi, mara nyingi ni vigumu kuamua kuhusu kiasi gani cha uzingativu umpe mtoto mmoja na kiasi gani kwa watoto wote.
  • Utafanya nini ili kujenga uhusiano mkubwa kadri inavyowezekana wakati unafanya kazi zako za vitendo?
ORODHA KWA AJILI YA KUJENGA UELEWA
  • Kwa nini walezi wataalamu ni watu muhimu sana kwa maisha ya watoto yatima?
  • Ni kitu gani muhimu unapolenga shughuli za kazi?
  • Ni kitu gani muhimu unapolenga kujenga uhusiano kazini?
  • Ni kitu gani kigumu katika kufanya vyote viwili kwa wakati mmoja?

Angalia “Vitu tunavyoweza kuvifanya sasa” kama tunataka baadhi ya mapendekezo kabla ya mada B: 

Chunguza na andika, au tumia simu ya mkononi au kamera kurekodi: unafanyaje kazi zako za vitendo kila siku. Angalia video na jadili namna unavyoweza kujihusisha na watoto wakati unafanya kazi za vitendo. Zingatia na jadili ni kwa vipi wakati mwingine unaweza kuona kazi za vitendo kuwa muhimu sana, na kwa vipi wakati mwingine unaweza kuona kujenga uhusiano kazini kuwa muhimu zaidi katika hali mbalimbali wakati wa mchana.

“Sifanyi uamuzi wowote kati ya kushughulikia watoto na kufanya kazi tena. Katika somo hili, nimejifunza kufanya vyote kwa wakati mmoja. Nina furaha, na mtoto wangu ana furaha, pia. Kwa namna hii, ninaweza kucheza nao michezo na wanaweza kunikumbatia. Kwa Namna hii, wanajua kwamba nitakuwa nao kwa namna yoyote ile”
 Kauli ya mlezi