Somo la 6/15

Ukurasa wa 4/4 Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Angalia na andika, au tumia simu yako au kamera kurekodi: jinsi unavyofanya kazi zako kwa vitendo kila siku. Tazama video na jadili jinsi unavyoweza kuihusisha na watoto wakati unafanya kazi kwa vitendo. Tambua na kujadili jinsi ambavyo wakati mwingine unaweza kuona vitendo kuwa muhimu sana, na namna wakati mwingine unaona kazi ya kujenga uhusiano ni muhimu sana katika mazingira mbalimbali wakati wa mchana.

Ufuatao ni mfano wa kile unachopaswa kufanya kabla ya somo linalofuata:

  • Chagua moja kati ya ujuzi na jadili jinsi utakavyoboresha kazi hadi somo linalofuata.
  • Amua ni mazoezi yapi utajaribu kuyaboresha na shughuli gani/muda wa mchana utayafanya
  • Panga namna utakavyofuatilia au kurekodi video ya mafanikio yako. Anza kwa kufuatilia mazoezi yako ya kawaida na namna watoto wanavyoitikia, na mazoezi yako mapya na namna watoto wanavyoitikia.
  • Andika kile ambacho mmejadili na kuamua kukifanya na nani atakifanya.

Asante kwa utayari wako na kila la heri katika kazi yako hadi somo linalofuata!