Somo la 7/21

Ukurasa wa 2/5 Utangulizi wa Mada: Jinsi watoto wanavyoonyesha hisia ya kupoteza wazazi

Utangulizi wa Mada: Jinsi watoto wanavyoonyesha hisia ya kupoteza wazazi

Kutegemeana na umri ambapo mtoto anaachanishwa na wazazi na kuwekwa katika ulezi, watoto huonyesha hisia na kuonyesha huzuni zao katika namna tofauti. Pia wana namna tofauti za kujaribu kustahimili huzuni zao. Watu mara nyingi wanasema kuhusu kupoteza mzazi kwamba “muda utatatua tatizo”, lakini kwa kawaida hili ni kweli tu kwa watoto ambao walikuwa wadogo sana wanapoachana na mzazi au mtu mwingine muhimu wa karibu. Kupoteza mzazi sio lazima kuwa kifo cha mzazi, bali hata kutenganishwa kwenyewe kwa kutoonana. Pia mzazi anaweza kuwepo lakini ashindwe kumhudumia kwa mfano, kutokana na msongo mkubwa wa mawazo wa mama mjamzito, magonjwa ya akili, au ukosefu wa matunzo katika utoto wa mlezi mwenyewe.
Muda na ukubwa wa kuonyesha hisia pia unategemea ni mawasiliano yapi wanayatoa walezi wapya.
HATUA YA KUONYESHA KUTOKUBALIANA NA HALI – ZOEZI LA KUMTAZAMA MTOTO KIMYA
Kwa kawaida watoto watapitia katika hatua ya kutokubaliana na hali wanapoachana au kutoonyesha hisia kwa: kulia, kukosa raha na ni vigumu kuwabembeleza, wanaweza kukataa jitihada za ukaribu kutoka kwa wazazi wao walezi wapya. Kwa hakika hizi ni hisia za kawaida na nzuri: mfumo wa ukaribu na mtoto unachochewa na kutenganishwa kama inavyopaswa ili kuzuia kutenganishwa zaidi.

Unaweza kuona ufafanuzi wa hisia hizo katika “Zoezi la Kutazamana Kimya” la Dkt. Edward Tronick. Kwanza, mama anaitikia na kuonyesha ushirikiano – kisha anaambiwa kutuliza uso wake. Mtoto mchanga mara moja anaanza kujaribu kupata uzingativu wake, anakata tamaa na hatimaye analia. Unaweza kufikiria jinsi mtoto mchanga pamoja na mama ambaye hawezi kuitikia anavyoweza kupata hali ya wasiwasi kupita kiasi.

HISIA KALI ZA KUTENGANISHWA KWA WATOTO MIEZI 0-24: KUONDOLEWA AU WASIWASI WA KUTENGANISHWA KWA UJUMLA

Ukosefu wa tabia ya uhusiano wa karibu:
Kama mtu wa karibu hatakuwepo baada ya kutenganishwa, au kama walezi hawatasikiliza mtoto anapolia, mtoto anaweza kuacha kulia na kuonekana kutulia, kutojali na kujitenga. Hakika hii ni dalili ya hatari: zoezi la mfumo wa kuwa karibu linaweza kusimama, lakini mtoto anaweza kuwa kwenye hali ya kudumu ya huzuni. Anaweza kuitikia kidogo au kutoitikia kabisa kwa matunzo na jitihada za kutoa ukaribu na kuliwazwa. Hili linaweza kuleta hali ya msongo mkubwa wa mawazo na kujitenga, ambapo mtoto hastawi au kukua ipasavyo. Hisia hizo ni za kawaida kwa watoto ambao wamekutana na mabadiliko mengi katika watu wanaowalea au kuwa nao karibu, na watoto ambao wamechanganyika na watu kidogo sana katika vituo vya kulelea watoto yatima au hospitali.

 

Kuathiriwa kupita kiasi kutokana na utenganishwaji
Au, kama kutenganishwa kumekuwa ni kwa ghafla na kwa kushtua sana – huenda mtoto anakuwa amechukuliwa na mamlaka au polisi wakati wazazi walipokuwa wanalia au wanagombana – mtoto anaweza kujenga hali ya jumla ya msongo na wasiwasi wa kutenganishwa. Huenda mfumo wa kumuachanisha mtoto umekuwa wa busara sana na “usio wa kawaida” kutokana na mshtuko mmoja au zaidi ya mapema. Hivyo, kila wakati unapoondoka chumbani au hata kugeuka, mtoto anaweza kuogopa na kuwa na hofu sana, na kuhitaji uthibitisho kwamba hutaondoka. Watoto wanaokuwa na wasiwasi usio wa kawaida katika kutenganishwa wanaweza kukung’ang’ania wakati wote, kuwa na matatizo makubwa ya kulala na kuhitaji kuondolewa shaka na kuliwazwa kwa muda mrefu hata baada ya kutenganishwa kwa muda mfupi na kwa kawaida. Hili ni tatizo la mara kwa mara katika awamu ya kwanza kwa watoto wanaowekwa katika ulezi.

 

MASWALI YA KUTAFAKARI NA MAZUNGUMZO
  • Je, uliona kujitenga au hofu kubwa ya kutenganishwa kwa mtoto wako unayemlea baada ya kupangiwa mahali pa kuishi?
  • Je, hali hiyo ilichukua muda gani (kama iliacha au kama haina nguvu kwa sasa)?
  • Iliathiri vipi hisia zako kwa mtoto?
  • Je, ulihisi huzuni au kujikataa mwenyewe kama mlezi wa mtoto?
  • Je, hofu kubwa ya mtoto ya kutenganishwa ilikufanya uogope kujaribu kutenganishwa naye kwa muda mfupi, kama vile kumuacha mtoto mchanga peke yake kwa muda mfupi?
  • Uliitikiaje kama mtoto hakukuitikia, au alikung’ang’ania mara kwa mara na kuogopa kuondoka kwako chumbani?