Session 9/19

Page 2/10 How to identify an attachment pattern – an experimental method developed by Mary Ainsworth

Unabainishaje taratibu za kujenga uhusiano wa karibu- njia ya majaribio iliyoanzishwa na Mary Ainsworth

Katika umri wa awali kabisa, watoto hujenga baadhi ya mikakati ili kujenga uhusiano wa karibu na walezi wao. Mikakati hiyo huitwa utaratibu wa uhusiano wa karibu na inaweza kugawanyika katika makundi manne. Usalama, ukwepaji, ukinzani na kutokuwa na utaratibu mzuri. Katika video hii utaona jinsi watafiti wanavyofuata baadhi ya mazungumzo kati ya watoto na watu wazima na jinsi hisia za kutengana kwa baadhi ya watoto zinavyoonyesha aina ya utaratibu wa uhusiano wa karibu walioujenga na walezi wao. Mfano wa kwanza uliotolewa katika video unaonyesha hisia za mtoto zilizo salama kunapotokea utenganishaji. Mfano wa pili unamuonyesha mtoto mwenye mbinu ya uepaji. Kwa sababu za kimaadili, hakuna rekodi ya watoto wakiwa katika hali ya kutofuata utaratibu.

Video hii inaweza kupatikana katika tovuti ya johnbowlby.com au katika YouTube