Somo la 9/19

Ukurasa wa 4/10 Tabia tatu za uhusiano wa karibu usio salama

Tabia tatu za uhusiano wa karibu usio salama

Sasa tutaangalia mifano mitatu ya tabia za uhusiano wa karibu usio salama na kujadili namna ya kutambua na kukabili kila hali iliyotajwa hapo chini:

Kila moja kati ya aina ya mbinu hizi za Uhusiano wa karibu inaweza kuelezewa kwa kina zaidi au kwa kiwango kidogo. Hivyo, kuna nafasi ambayo mtoto wako ataonyesha tabia tofauti chache.
Wazazi walezi walio wengi wanajikuta kwamba wanakutana na kukataliwa au hasira – hata kama wanakuwa tabia ya mlezi salama. Kwa hali hii nadharia ya Bowlby katika modeli ya ‘ufanyaji kazi wa ndani ya mtoto’ ilithibitisha kufaa sana. Katika uhusiano wake wa awali na watu wazima mtoto amejenga hali ya matarajio ya hisia ambayo yanadhibiti tabia yake ya kuchangamana. Mtoto anaweza kutojibu au kutoonyesha hisia kwa vitendo vyako vya kumpatia matunzo mazuri na ya upendo kwake kwa sababu anaweza kuwa na matarajio tofauti yaliyojengwa na uzoefu mbaya wa awali, kwa mfano kudanganywa, kutendewa vibaya, kutowajibika, n.k.

Kielelezo kinatoa mfano wa mlezi akifanya tabia ya matunzo salama lakini anakutana na uzoefu wa awali wa mtoto kutokuwa salama, ambao umejenga modeli ya ufanyaji kazi wa ndani ya mtoto unaoweza kuchukua muda mrefu. Hata hivyo, unaweza kukamilishwa kwa uzoefu mzuri unaojirudia katika uhusiano wa matunzo.