Somo la 9/19

Ukurasa wa 6/10 Tabia isiyo salama ya ukinzani wa kuwa na uhusiano wa karibu

Tabia isiyo salama ya ukinzani wa kuwa uhusiano wa karibu

Kama mtoto au mtoto mdogo amekutana na mlezi ambaye hatabiriki kabisa, ambaye mara nyingi huadhibu au kukaripia, ambaye ni mwema katika muda mfupi na kuonyesha hisia nzuri na mbaya mtoto anaweza kujenga mbinu ya ukinzani wa kujenga uhusiano wa karibu. Mtoto anajielekeza katika kutaka huduma na wakati huohuo anakuwa na hofu kubwa ya mlezi asiyetabirika. Utaratibu huu unaonekana mara nyingi kwa watoto: Kama walezi wa awali walikabiliwa na upotevu mkubwa wa walezi muhimu katika makuzi yao, kama kuna migogoro au ukatili wa mara kwa mara kati ya walezi au kama mlezi ana ugonjwa wa akili.
Katika matukio yote haya tabia ya mlezi haitatabirika kwa mtoto.

  • Mtoto atamng’ang’ania mlezi wakati wote, na haridhiki na ni vigumu kumbembeleza.
    – Hatakuwa na usalama wa kutosha kuanza kucheza, na atakuwa amejawa na hofu ya kutenganishwa.
    – Atajaribu kumdhibiti mlezi na “kuchukua jukumu”.
  • Watoto wakubwa watakuwa na woga mkubwa kuhusu yale ambayo wengine wanaweza kufanya au kufikiria, katika njia mbaya (“hawanipendi”, “unaichukia”).
  • Wakati fulani mtoto atajaribu kuwadhibiti wengine, atajaribu “kuwa mzazi” wa watoto wengine katika njia ya kuwadhibiti. Wakati mwingine mtoto anaweza kulalamika sana kuwa anaumwa au kutoeleweka au kutopendwa na mtu yeyote. Anaweza kubadilisha uamuzi wako wote au kuendelea kujaribu kujadili hali yoyote.
  • Hatakuwa na urafiki mzuri na wenzie wengi, lakini atajaribu kung’ang’ania rafiki mmoja (“Wewe tu ndiye rafiki yangu, kama utazungumza na wengi utakuwa umenisaliti”).
  • Katika mazingira yaliyopita kiasi mtoto anaweza kuwa katili na kujaribu kuwafanya watoto wengine kufanya vitu au shughuli ambazo hawazipendi au hawazitaki, kama vile unyanyasaji kingono au vitendo vya kikatili.
  • Mtoto anaweza kuhitaji uangalizi, lakini wakati huohuo hapendi au anachukia au kuendelea kuwakosoa walezi. Anaweza kujaribu kuwatenganisha walezi (“Ninakutaka wewe tu, ninamchukia yule”).
  • Mtoto ataendelea kuzingatia katika uhusiano mbaya na kujaribu kuepuka au kujadili kazi yoyote.
MATUNZO YA KITAALAMU DHIDI YA TABIA ZA WATOTO WENYE UKINZANI
Kama mtoto anahitaji uangalizi – na wakati huohuo anawaogopa sana walezi – ukaribu na imani vinakuwa ni tatizo, na kurekebisha umbali na ukaribu wa hisia linakuwa ni tatizo. Watoto hawa wanaumia sana unapaswa kuzingatia kuwafanya wajisikie salama kwa:

  • Kuwa mkarimu, lakini pia kuwa imara. Usimuadhibu mtoto, sisitiza kwa upole kuhusu mahitaji na masharti yako.
  • Fanya uamuzi ambao mtoto hawezi kuufanya.
  • Msaidie mtoto kuzingatia kile anachokifanya: “Sasa tunasoma, hatutafanya jambo jingine lolote kwa dakika 10 zijazo”.
  • Andaa utaratibu unaotambulika wenye shughuli fupifupi, na urudie kila siku.
  • Wakati mtoto anapokushutumu au kukulaumu, uwe mpole na mwema lakini usijadiliane kuhusu uamuzi wako. Kama ukiwasilisha mahitaji, hakikisha kwamba hukati tamaa au kuanza kutoa sababu kuhusu mahitaji hayo. Wakati mtoto anapotishwa na mazingira, msaidie kuona uhalisia katika mazingira na hali halisi: “Unasema unataka kufa kwa sababu hakuna anayekupenda – sawa, una huzuni na hasira sasa – vitaisha muda si mrefu- hata kama hufikirii hivyo sasa.”
  • Jaribu kutambua na kuzungumza na walezi wengine kuhusu wakati mtoto anakufanya ukasirike na kuwa na ukinzani. Jaribu kuwa mbali kwa namna unavyomwangalia mtoto, ili kuwa mtulivu, thabiti, mwema na mwenye msimamo.
TAFAKARI
  • Je, unamuona mtoto yeyote unayemlea akifanya hivyo?
  • Unafanya nini mtoto anapokujibu, kujaribu kuwafanyia ukatili wengine au anapolalamika au kukushutumu?
  • Je, unamkumbuka mtu yeyote katika familia/marafiki zako anayefanya kama hivi?
  • Kuna ugumu gani kwako katika kukabiliana na hali wakati watoto wanapokuwa na tabia ya ukinzani?