Somo la 9/21

Ukurasa wa 7/10 Tabia isiyo salama ya kutofuata utaratibu wa kujenga uhusiano wa karibu

Tabia isiyo salama ya kutofuata utaratibu wa kujenga uhusiano wa karibu

Baadhi ya watoto wamekabiliwa na viwango hivyo vya hofu na woga kwa walezi wao ambao hata mbinu zao za kujitenga na ukinzani zilishindwa. Hali hii inaitwa tabia ya kukanganya na ya kutofuata utaratibu, na inaweza kujitokeza kwa muda mfupi au kuwa ya kudumu. Inapotokea mtoto anafanya hivyo, anakuwa na wasiwasi kwamba amepoteza njia ya uwiano wa kukabiliana na urafiki wa karibu na kutenganishwa. Tabia hii imeonekana mara nyingi kama hakuna yeyote aliyechochea au kumjali mtoto mapema katika maisha yake, kwa mfano kama mama mwenyewe alitelekezwa vibaya alipokuwa mtoto au kama wazazi walikuwa watumiaji wakubwa wa dawa za kulevya, au waathirika wa vita na migogoro wakati mtoto wao alipokuwa mdogo.
 

Mtoto au mtoto mdogo anaweza:

  • Kuwa na tabia ya woga dhidi ya mlezi hata kama mlezi anamtendea kwa usalama.
  • Wakati wote anajiondoa, kwa mfano anapopakatwa katika mapaja ya mlezi.
  • Kujibu kwa namna za ajabu:
    • Mtoto anaweza kuwa mkali kwa kuogopa wakati mlezi anapoingia,
    • Kukaa kando ya mlezi na kuepuka macho kukutana,
    • Kulalamika katika njia ya ajabu bila kukusudia kukutana na mtu yeyote, kurudia sauti au maneno yaleyale ya ajabu wakati wote,
  • Au kuwa na tabia ya kuvuruga ghafla utafutaji wa uangalizi: Anaweza kuanza kugusana na wewe, lakini ghafla anaanza kufanya jambo jingine katikati ya kugusana, kama vile kucheza au kujaribu kukupiga. 

 

Mtoto mkubwa au kijana anaweza:

  • Kukutana kwa muda mfupi au kwakwa kutojali watu na vitu.
  • Kutokuwa na utulivu na kutozingatia au kulenga watu na vitu. Kuanza shughuli mpya lakini kutozimaliza wala kuzifurahia.
  • Kutokuwa na hisia za mipaka binafsi (kuzungumza kuhusu mambo ya ndani au binafsi kwa watu asiowajua)
  • Kuonyesha ushirikiano usiokuwa na ubaguzi (kuzungumza na mtu yeyote anayekutana naye, kutafuta faraja kwa urafiki wa karibu na watu wageni kabisa). Labda hata wakionyesha tabia ya kutochagua jinsia.
  • Kukosa hisia za hatia, kujuta au kutubu.
  • Anaweza kuwa mkarimu sana na kuwa na uhusiano na watu wengi, lakini mtoto hana marafiki wa muda mrefu au wenye uhusiano wa ndani na walezi maalumu.

 

Katika matukio mabaya, mtoto anaweza kujenga “Tatizo la kutokuwa na ukaribu” akiwa na miaka 5-7:
Mtoto hawezi kushirikiana na wenzie katika njia ya uwazi, na hana uwezo wa kujenga uhusiano na wengine unaoweza kudumu kwa muda mrefu. Kukosekana huku kwa mbinu ya uwazi ya uhusiano wa karibu ni tatizo kubwa, na watoto wenye tabia hii mara nyingi hujenga tatizo la kutojijali wanapokuwa wakubwa kama vile “Kutokubalika”, “Tatizo la tabia ya kutochangamana”, n.k.).

MATUNZO YA KITAALAMU DHIDI YA TABIA ZA WATOTO ZISIZOFUATA UTARATIBU
Kama mtoto amepitia hali ya kukosa mahitaji muhimu na mabadiliko yasiyokuwa na utaratibu katika uhusiano wake na walezi wa awali, kila kitu “kimecheleweshwa”. Misukumo na upotofu mwingi unaweza kusababisha ukuaji wa mtoto kuwa taratibu, hususan kuhusiana na ukuaji wa kijamii, kihisia na kiakili.
Hivyo unaweza kumuona mtoto mdogo anaonekana mkubwa kuliko umri wake:

 

  • Gawa umri wa mtoto kwa tatu – ni aina gani ya uhusiano ni mzuri kwa mtoto wa umri huo, mtoto anaelewa maelekezo kwa kiasi gani, mtoto wa umri huo anaweza kuzingatia jambo kwa muda gani?
  • Unapaswa kujiuliza mwenyewe: Matatizo ya mtoto huyu yanakuwa ya kawaida kwa mtoto wa umri gani?
  • Unapaswa kupendelea uhusiano wa mlezi binafsi kwa kadiri iwezekanavyo, kabla hujahitaji uhusiano wa mtoto na watoto wenzie.
  • Kupendelea shughuli na mazungumzo ambayo yanawahusu watoto wadogo.
  • Kuwa mvumilivu sana na kutokuwa na matarajio makubwa kwa maendeleo ya haraka.
  • Katika shughuli za kila siku unaweza kufanya kile ambacho watoto wanajifunza kutoka kwa mama zao:
    • Endeleza kutazamana machoni, uwe na mazungumzo ya kutosha, kugusana mwili zaidi.
  • Unapaswa kupanga shughuli fupi fupi na mpango kazi wenye utaratibu mzuri wakati wa mchana.
TAFAKARI
  • Je, unamuona mtoto yeyote unayemlea akifanya hivyo?
  • Unafanya nini wanapofanya kwa namna ilivyoelezwa?
  • Je, unamkumbuka mtu yeyote katika familia/marafiki zako anayefanya kama hivi?
  • Kuna ugumu gani kwako katika kukabiliana wakati watoto wanapokuwa na tabia ya kujitenga?