Somo la 9/19

Ukurasa wa 8/10 Maoni ya jumla ya matunzo ya kitaalamu na Uhusiano wa karibu

Maoni ya jumla ya matunzo ya kitaalamu na Uhusiano wa karibu

Watoto wanaolelewa wako katika hatari kubwa ya kujenga tabia isiyofaa au uhusiano usio mzuri. Wanakosa mawasiliano na wazazi waliowazaa, kubadilishwa kwa walezi mara nyingi wakiwa wadogo wakati wa mchana. Mara nyingi wanakuwa katika kunyanyaswa au ukosefu wa vitu kabla ya kuingia katika ulezi au familia ya ndugu.
(Kwa uelewa zaidi kuhusu wanavyotendewa , tafadhali angalia kitabu hiki kuhusu utendewaji kilichotafsiriwa katika lugha nyingi www.attachment-disorder.net).

Unaweza kufanya nini katika ulezi wako kwa watoto hao, na unatarajia matokeo yapi?
Hii labda inategemea sana umri wa mtoto anapopelekwa katika matunzo ya wataalamu. Utafiti wa watoto wanaolelewa unaonyesha kwamba kama mtoto ni mdogo chini ya miezi 20 wakati anapelekwa mahali pa kuishi, atabadilisha utaratibu wake wa Uhusiano wa karibu kwa Yule mlezi mtaalamu, ikiwa mtu huyu atamjali mtoto kwa muda wake mwingi wa kazi.
 Hii inamaanisha kwamba kama utafanya matunzo salama, mtoto anaweza kuwa na ukaribu mzuri.

Kwa watoto ambao ni wakubwa wakati unawapokea kwa matunzo, ni vigumu zaidi kufanya mabadiliko ya msingi katika tabia yao ya Uhusiano wa karibu, unapaswa kuwa mvumilivu zaidi, na kwa kiasi fkukubali kwamba mtoto huyu anahitaji msaada wa ziada ili aweze kufanya kazi vizuri (Kwa uelewa zaidi angalia baadhi ya machapisho ya Mary Dozier, Delaware University at www.psych.udel.edu/people/detail/mary_dozier).