Somo la 13/19

Ukurasa wa 4/5 Mada B: Namna ya kufanya mawasiliano na wazazi - uhusiano na mipango

Mada B: Namna ya kufanya mawasiliano na wazazi–uhusiano na mipango

Kuna mambo mawili ya kuwasiliana na wazazi: Usimamizi wa uhusiano wa kijamii na mipangilio kwa vitendo. Ni kwa vipi unaweza kumudu uhusiano wa kawaida na wazazi halisi? Kwa ujumla unapaswa kuwa na mtazamo mzuri kuhusu mawasiliano yote na wazazi na utekelezaji wake: 

  • Uelewa na kukubali mtazamo:“Ninaelewa kwamba uliamua au uliacha kumlea mtoto wako. Sikulaumu kabisa, nafikiri umechukua uamuzi wa kuwajibika kwa kumleta kwetu sisi, na nina furaha kwamba umemkabidhi mtoto kwenye ulezi wetu. Uwe na uhakika kwamba tutafanya kila tunaloweza kuendelea kuwasiliana na kushirikiana na wewe”.
  • Tumia vipimo vitano vya huduma salama (angalia Somo la 5): Uwe unatabirika: kuwa makini, soma hali ya wazazi na tekeleza kutokea hapa, kuwa tayari kuwafariji, Pata hisia kama za wazazi lakini si kwa namna hiyo hiyo kama wazazi. Zungumza kuhusu hisia na nia, kwa mfano: Ninaelewa kwamba wakati mwingine unapata wivu na kutukemea sisi. Lazima huwa ni shida kuona mtoto wako kwenye malezi ya wengine wakati unatamani kama ungeweza kufanya hivyo mwenyewe. Wazazi wote hufanya hivyo, wakati mwingine ninaona wivu dhidi mwalimu wa mtoto wangu mwenyewe – mara zote anazungumza namna anavyompenda wakati muda wote anatukosoa sisi kama wazazi!”
  • Wakati hasa mtoto aliye chini ya ulezi wako akiwepo: ongea vizuri kuhusu wazazi na kuogea vizuri na hao wazazi: “Nina furaha sana mama yako yupo hapa kukuona, ana sauti nzuri sana, n.k.”.
  • Ukiwa na wazazi wa kawaida ambao waliacha kumlea mtoto wao mara nyingi unaweza kufahamiana nao, labda hata kabla ya kuwa marafiki na unapaswa kujitahidi kujenga uhusiana na wazazi mkiwa na lengo moja la kumsaidia mtoto wao kukua. Unapaswa kuwaambia kuanzia mwanzo kwamba huna lengo la kumchukua moja moja mtoto kutoka kwao.

 

KUSIMAMIA ZIARA NA MAWASILIANO YA WAZAZI WENYE MATATIZO
Baadhi ya familia zilizokabidhiwa mtoto kumlea huvunjika au huingiliwa – si kwa sababu ya matatizo ya watoto wanaowalelea, lakini mara nyingi kwa sababu ya matatizo ya usimamizi wa mawasiliano na wazazi wenye matatizo. Mawasiliano haya wakati mwingine huwa chanzo cha msongo wa hisia na mkanganyiko kwa familia yote iliyokabidhiwa mtoto kumlea.

Zifuatazo ni kanuni na mapendekezo kwa ajili ya usimamizi wa hali ya mawasiliano kama vile ziara kutoka kwa wazazi halisi na mazingira ambayo familia zote mbili zinakutana:

1. Kuwa ” mzazi wa mzazi”:
Unapaswa kuwaona wazazi wachanga sana labda si kama wazazi, lakini pia kama “watoto”ambao kwao kazi ya uwajibikaji wa kulea kwao ilikuwa ngumu sana. Hii ina maana kuwa maisha ya awali ya wazazi wenyewe yalikabiliwa na msongo kwa sababu wenyewe hawakuwa wamekua, lakini labda inaweza kuwa ni msukumo au kutowajibika kama ilivyo kwa vijana, hata kwa siku nzuri.
Ushauri mmoja wa kutekeleza ni huu: Gawa umri wa wazazi kwa tatu au nne kuhusiana na stadi za kijamii. Hivyo, unapaswa kuelewa kwamba utafanya kama mzazi kwa wazazi, panga ziara kwa ajili yao, kuwa mvumilivu, usikasirike kama waliahidi kumtembelea mtoto na kusahau, na tulia kama watapiga kelele kwa sababu kitu kidogo huwa kinawakasirisha.

2. Mtumie mfanyakazi wa huduma za jamii au msimamizi kwa kutengeneza muafaka wa mawasiliano:
Ni mara nyingi kiasi gani kunapaswa kuwa na ziara au mawasiliano itaamuliwa na mamlaka, na hili si jukumu lako. Unaweza kuwasiliana na mamlaka kama unafikiri ratiba haikufai wewe au mtoto. Kama wazazi watajaribu kukuendesha au kutaka mawasiliano zaidi ya yale yaliyokubaliwa, usianze kubishana. Wewe waambie kwamba hili haliamuliwi na wewe, isipokuwa mamlaka na ni mamlaka tu inaweza kubadilisha muafaka wa mawasiliano.

BAADHI YA USHAURI WA JUMLA UNAOHUSIANA NA WAZAZI WENYE MATATIZO
Kanuni 4 za kusimamia ziara za wazazi wenye matatizo:

A. Panga utaratibu kuanzia siku ya kwanza na kuwa imara, mwelekezaji, mkarimu na muwazi. “Karibu nyumbani kwetu. Nitawasaidia kuifanya ziara hii kuwa na uzoefu mzuri hivyo kitu cha kwanza tunachofanya, ni kwamba wote tukae chini pale jikoni, nitakapokuwa nawatengenezea kikombe cha kahawa, kaeni mtulie”. Hii inaonyesha kwamba unachukua nafasi ya uongozi kuanzia mwanzo, ambayo ni muhimu kama wazazi wana hofu, hasira au wanahisi kutokuwa salama.

B. Tengeneza ratiba ya kile kinachokwenda kutokea wakati wa ziara na wasilisha mpango wa shughuli kwa ajili ya kazi za kufanya. Inaweza kuwa ya kuchosha kwa pande zote mbili kwamba, ” mkae na kuongea kikawaida” bila ratiba. Ni rahisi zaidi kulenga kitu ambacho mtafanya kwa pamoja: Sasa, wakati tunakunywa kahawa nitawaambia tutafanya nini leo: kwanza tutaoka keki kwa pamoja ili kwamba tuweze kucheka na kuwa na muda mzuri na mtoto wako. Kisha tutakuwa na mapumziko mafupi, ambako tungeweza kutembea kidogo hapo jirani au kucheza mchezo kidogo. Kisha tutazungumza namna mtoto anaendelea, na nitawaonyesha michoro yake. Baada ya hapo wote tutaagana, na anaweza kusubiri ziara yenu inayofuata. Naweza kuwasindikiza kwenye kituo cha basi kama mnapenda”.
Mazungumzo haya yanatolewa kwa njia ya maelekezo na kwa ukarimu ukionyesha wazazi namna unavyowalea: kujali, kazi za vitendo na kuwaonyesha namna unavyotaka wajiheshimu kwa kina. Wazazi wenye matatizo wana shida ya kuhisi mipaka ya kawaida, hivyo unapaswa kuwa wazi na usiyetaka makuu namna unavyowaelekeza kuhusu mawasiliano. Kwa mfano: “Kama unataka kuongea na mimi kwenye simu, Ninapatikana kutoka (saa xx hadi saa yy) kila siku. Kama ukipiga simu nje ya muda huu sitapokea simu yako kwa sababu nitakuwa nafanya kazi ndani au nawahudumia watoto”.

C. Ziara za muda mfupi kwa kawaida zinafanikiwa zaidi kuliko zile za muda mrefu. Msongo wa hisia ya hali inamaanisha kwamba wazazi wenye matatizo wanaweza kujidhibiti wenyewe kwa muda mfupi tu. Kama saa 4 za ziara zitaishia kwenye maafa na ugomvi, ni vizuri zaidi kufanya zaidi ziara za saa moja ili kuona kama hii itafanya kazi vizuri zaidi. Hili linaweza kuwa pendekezo lako kwa mamlaka ambao wanasimamia familia iliyokabidhiwa mtoto imlee.

D. Kuwa mzazi wa wazazi wakati wa ziara. Mara nyingi wazazi wenye matatizo na wazazi ambao hawajaveka wanaweza kuona vitu kwa mtazamo wao tu na ama wakawa na matatizo ya kuwasiliana na mtoto wao au wanaongea kuhusu mahitaji yao tu. Hakuna haja ya kueleza upande wenye matatizo wa wazazi kwa kuwatarajia kuhusiana na mtoto wao wakati wa ziara nzima – hii inaweza kuwa usumbufu kwao. Kwa hiyo kwa baadhi ya ziara, kwa mfano, baba mlezi anaweza kuongea na wazazi, wakati mama mlezi akimwangalia mtoto. Wazazi wenye matatizo mara nyingi wanakabiliwa na matatizo yao wenyewe kuliko yale ya mtoto, na unapaswa kukubaliana na hili. Hii ni sehemu ya tatizo lililosababisha mtoto kupelekwa mahali pa kulelewa.