Somo la 19/19

Ukurasa 1/5 Ujuzi wa kitaalamu kutokana na mchakato wa kujifunza

Ujuzi wa kitaalamu kutokana na mchakato wa kujifunza

Ujuzi unaotakiwa kutumika

  • Kufanya tathmini ya mpangilio wa maendeleo yenu kama wazazi walezi

 

Mada ya somo:

Katika somo la 15 utajifunza matokeo ya kazi yako kutokana na mafunzo haya katika maeneo manne tofauti:

  • Maendeleo ya jumla ya mtoto wa kulea na uhusiano wa mtoto/mlezi
  • Ustadi wa wazazi walezi kuhusiana na nadharia na vitendo katika malezi ya mtoto
  • Uhusiano kati ya wazazi walezi na mtandao wa kila siku wa jamii
  • Uhusiano na mazingira ya jirani na watoa maamuzi.

 

Malengo ya somo:

Kulinganisha hali ya ulezi wako mwanzoni mwa mafunzo na hali yako ya sasa katika maeneo manne tofauti yaliyotajwa hapo juu. Unapolinganisha mahali pa kuanzia pa mafunzo haya ya Fairstart na hali yako ya sasa:

  • Mafunzo yaliathiri vipi uwezo wetu wa kutunza watoto wanaolelewa?
  • Je, umeunda familia mlezi ambayo wanajumuika pamoja, wataalamu zaidi katika namna yao ya kufanya kazi na uwezo zaidi wa kutoa ulinzi wa kitaalamu kwa watoto?
  • Mafunzo na malezi yako yalikuathiri vipi kama familia?
  • Kama ni mzazi pekee mlezi, tafadhali tafakari – wewe mwenyewe – kuhusu maendeleo na ujuzi wako binafsi.