Somo la 6/21

Ukurasa wa 1/4 Namna ya kutoa malezi ya kitaalamu: Mwelekeo wa uhusiano wa karibu

Unatoaje malezi kitaalamu na watoto wanaipokeaje huduma hiyo: Mambo yanayoambatana na huduma. Mwelekeo wa uhusiano wa karibu

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

•  Elewa uwiano uliopo kati ya Shughuli za Kazi na Uhusiano katika Kazi.
•  
Ujuzi wa kuhudumia kwa Mwenendo wa Kitaalamu wa Ulezi Salama.
• 
Kutambua na kufanya kazi kwa Mtindo wa Ulezi Salama.

Mada ya somo:

Katika somo la 4 umejifunza kuelewa tabia zinazojenga ukaribu na namna walezi wanavyoweza kuwapa watoto Msingi Salama. Katika mafunzo haya utajifunza kwa kina kuhusu Mwenendo salama wa mlezi, na namna watoto wanavyoipokea huduma wanayopewa. Walezi wanatakiwa kuwa na tabia gani ili kuwafanya watoto wahisi kuwa salama, hivyo kwamba wanaweza kuchangamana, kucheza na kujifunza? Pia, watoto hujifunza mapema sana namna ya kukabiliana na kutenganishwa. Mtoto mmoja mmoja hujifunza mkakati wa kumudu utengano na msongo kutoka kwa walezi wa kwanza. Kimsingi watoto wana njia nne za kuwafanya wakabiliane na halii hiyo – mikakati hii inajulikana kama Taratibu za Uhusiano wa Karibu. Utajifunza kutambua taratibu hizi, na kuwa na mapendekezo ya namna ya kutoa mwitikio katika kuchangamana na mtoto.

 

Malengo ya somo:

Lengo kuu la somo hili ni kuelewa namna ya kutoa huduma kitaalamu.

Kwa nini na kwa namna gani:

Huduma za kitaalamu zinalenga kwenye kujenga uhusiano wa kihisia na kijamii na mtoto. Wakati huohuo pia unatakiwa kufanya mambo mengi kwa vitendo: kubadilisha nepi, kuandaa chakula, kulisha watoto, n.k. Kwa hiyo mtajadili pia namna ya kuwianisha baina ya kufanya kazi na kujenga uhusiano na kazi za vitendo. Tutajifunza kwa kina ni kitu gani muhimu cha kufanya katika uhusiano wa mlezi na mtoto.
Kabla ya kufikia kupata malezi, mtoto anaweza kuwa amewahi kutelekezwa au kuwa na wazazi wakatili, walezi wengi au wafanayakazi wenye shughuli nyingi na waliofanyishwa kazi nyingi. Kwa sababu hii, watoto wengi hawapokei huduma kikawaida na inaweza kuchukua muda mrefu kabla ya kufanya hivyo. Kwa hiyo, pia tutajifunza namna watoto wanavyoipokea huduma, taratibu zao za ukaribu, na namna unavyoweza kufanya ili mtoto ajisikie salama.