Somo la 5/21

Ukurasa wa 1/5 Mtindo wa Mlezi na ukuaji wa ubongo wa watoto wachanga na watoto wanaojifunza kutembea

Mtindo wa Mlezi na ukuaji wa ubongo wa watoto wachanga na watoto wanaojifunza kutembea

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

• Kuelewa ni sayansi ipi iliyogundua kuhusu matokeo chanya ya kugusana mwili mapema na kuchochea hisia.
Kupanga namna matunzo ya uchocheaji wa hisia yalivyofanyika katika utendaji wa kila siku, na namna hili linavyoweza kusaidia ukuaji wa ubongo – hususan kwa watoto wenye miezi 0 – 24.

Mada ya somo:
Katika somo hili la mafunzo utajifunza kuelewa umuhimu wa kugusana mwili na uchocheaji wa hisia kwa ajili ya ufanyaji kazi na ukuaji wa ubongo. Unaweza kuwa na mapendekezo kwa ajili ya utendaji na utaratibu wa kila siku ambao unasaidia ubongo kufanya kazi. Unaweza kuwa na mapendekezo kwa ajili ya kuchochea hisia za watoto wanaozaliwa kabla ya siku zao na watoto dhaifu.

 

Malengo ya somo:
Lengo la somo ni kuelewa umuhimu wa uchocheaji wa mapema wa hisia za mwili, na jinsi uchocheaji wa hisia unavyosababisha akili kufanya kazi. Katika ubongo wa mtoto aliyezaliwa, ufanyaji wa kazi katika ubongo unakuwa mdogo na haujawa thabiti, na ni uchocheaji wa mwili tu ndiyo unaweza kuamsha ubongo na kuuwezesha kufanya kazi. Kukosekana kwa shughuli za uchocheaji na mazoezi ya mwili ni hatari sana, hususan kwa mtoto mchanga na mtoto mdogo: inaathiri ukuaji wa kimwili, kiwango cha kuishi, hamu ya chakula na mmeng’enyo wa chakula, muda wa kulala, kinga ya mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa na kuchangamka kwa mfumo wa uhusiano wa karibu baada ya kuzaliwa. Kwa kutumia uelewa huu, utajifunza idadi kubwa ya vitendo vinavyoweza kuwa sehemu ya utaratibu wako, na utajadili na kupanga jinsi vitendo hivyo vinavyoweza kuwa sehemu ya maisha ya kila siku katika familia mlezi.