Somo la 11/19
Ukurasa wa 1/4 Mimi ni nani? Kujenga utambulisho mzuri kutoka kwenye historia iliyogawanyikaMimi ni nani? Kujenga utambulisho mzuri kutoka kwenye historia iliyogawanyika
• Stadi za kupanga na kutekeleza mazungumzo ya wazi kuhusu kuwa kwenye huduma ya ulezi.
• Jinsi ya kutumia uzoefu wako katika maisha kama mfano wa masimulizi.
• Jinsi ya kuwasaidia watoto na vijana kuelewa tabia zao kama athari ya mwitikio wa asili wa kupoteza wazazi.
• Jinsi ya kuandaa kazi za vitendo kwa ajili ya watoto, ambapo utenganishwaji mgumu kutoka kwa watu muhimu katika maisha yao unaweza kutatuliwa.
Maudhui ya somo: Katika mfunzo haya utajifunza kuwasaidia watoto kujenga wazo chanya kuhusu wao ni nani na hali ya kujiamini. Somo hili linatoa nyenzo za namna mtoto anavyoweza kuendana na hali ya kuwa na vyanzo tofauti vya uasili.
Malengo ya somo: Lengo kuu la somo hili ni kuwasaidia watoto kujenga wazo muhimu kuhusu wao ni nani kwa kuwasaidia kuelewa asili yao.