Somo la 7/19

Ukurasa wa 1/5 Kutoka katika hali ya maumivu kurejea katika hali ya kawaida: kuwasaidia watoto kukabiliana na hisia za kupoteza na kutenganishwa na wazazi

Kutoka katika hali ya maumivu kurejea katika hali ya kawaida: kuwasaidia watoto kukabiliana na hisia za kupoteza na kutenganishwa na wazazi

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

  • Ujuzi wa kupanga na kufanya mjadala wa wazi kuhusu kupoteza na kutenganishwa na wazazi
  • Namna ya kutumia uzoefu wako wa maisha kama maarifa kwa ajili ya hadithi za mfano
  • Jinsi ya kuwasaidia watoto na vijana kuelewa tabia zao kama mwitikio wa kawaida wa kupoteza wazazi.
  • Jinsi ya kufanya shughuli za mazoezi kwa watoto wadogo ambapo hali ya kupoteza wazazi inaweza kutatuliwa.

Mada ya somo:
Katika somo hili la mafunzo utatumia njia za kuwasaidia watoto kukabiliana na kupoteza wazazi, kwenda mbali na wazazi, na matukio mengine yanayowasilisha upotevu mkubwa au kutenganishwa kwa ghafla.

 

Malengo ya somo:
Lengo kuu la somo hili ni kufanya mijadala ya wazi na yenye taarifa nyingi na watoto na vijana kuhusu majibu ya kupoteza wazazi. Pia, jinsi ya kuandaa shughuli ambapo watoto wanaweza kukubaliana wenyewe na mazingira ya maisha yao wanapoishi bila ya wazazi.

Tafadhali tumia dakika 15 (au muda mwingi kwa kadiri unavyohitajika) kwa ajili ya kuhitimisha ulichokifanyia kazi kati ya somo la mwisho na hili la sasa:

•  Je, ulifanikiwa kukamilisha kile ulichokipanga?
•  Nini kilikuwa rahisi kukifanya na kipi kilikuwa kigumu?
•  Je, ulijifunza nini kwa kufanya ulichokipanga?
•  Kipi utafanya vizuri zaidi wakati ujao katika masomo?

Tafadhali kumbuka: Haina shida kama ulipata matatizo-hii ndiyo namna mpya ya kufanya kazi, inahitaji kufanyia mazoezi kabla haujazoea.