Somo la 9/15

Ukurasa wa 1/10 Namna ya kuelewa na kuboresha tabia ya kutokuwa na uhusiano wa karibu

Namna ya kutambua tabia ya kutokuwa na uhusiano wa karibu

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

•  Kutambua tabia isiyo salama ya kuepuka kuwa na uhusiano wa karibu kwa watoto.
•  
Kutambua tabia isiyo salama ukinzani ya kuwa na uhusiano wa karibu kwa watoto.
•  
Kutambua tabia isiyo salama ya kutofuata utaratibu wa uhusiano wa karibu kwa watoto.
•  
Kujua jinsi ya kukabiliana tabia hizi tatu za uhusiano na kuwafanya watoto wajihisi wako salama.

Mada ya somo:

Katika somo hili la mafunzo utaonyesha namna ya kutambua tabia ya mtoto ukirejea matatizo ya awali ya uhusiano wa karibu – namna ambavyo yatima wakati mwingine wanaweza kujenga tabia ya utaratibu usio salama wa uhusiano wa karibu. Unaweza kuwa na mapendekezo ya namna unavyoweza kufanya kazi na watoto wenye uhusiano wa karibu usio salama.

 

Malengo ya somo:

Yatima na watoto walioko nje na nyumbani mara nyingi wamekuwa wakikabiliwa na misukumo mingi ya awali; ingawa watoto wanaozaliwa njiti na wenye uzito mdogo, kunakoweza kuathiri ukuaji, kukosekana kwa ulezi salama kutoka kwa wazazi pamoja na matatizo katika maisha yao na shifti nyingi kwa walezi.

Tafadhali tumia dakika 15 (au muda mwingi kwa kadiri unavyohitajika) kwa ajili ya kuhitimisha ulichokifanyia kazi kati ya somo la mwisho na hili la sasa:

•  Je, ulifanikiwa kukamilisha kile ulichokipanga?
•  Nini kilikuwa rahisi kukifanya na kipi kilikuwa kigumu?
•  Je, ulijifunza nini kwa kufanya ulichokipanga?
•  Kipi utafanya vizuri zaidi wakati ujao katika masomo?

Tafadhali kumbuka: Haina shida kama ulipata matatizo-hii ndiyo namna mpya ya kufanya kazi, inahitaji kufanyia mazoezi kabla haujazoea.