Somo la 4/19

Ukurasa wa 1/15: Kuelewa Nadharia ya msingi ya Uhusiano wa karibu: Fursa yako kwa kazi za kitaalamu

Kuelewa Nadharia ya msingi ya Uhusiano wa karibu: Fursa yako kwa kazi za kitaalamu

Ujuzi unaotakiwa kutumika:

  • Ujuzi wa kutumia tabia ya uhusiano wa karibu kitaalamu.
  • Uelewa wa mwelekeo: “Kutafuta Msingi Salama” na “Ugunduzi”, na namna ya kusaidia na kuhamasisha majukumu haya mawili kwa watoto wachanga na watoto wadogo.
  • Kuelewa mwelekeo Mwenendo wa Mlezi wa Msingi Salama .

Zingatia: Mafunzo ya Somo la 4 ni nadharia ya uelewa wa msingi ambao kila mmoja anapaswa kuukumbuka.

Mada ya somo:

Katika somo hili utafanya kazi kwa umuhimu wa nadharia ya Uhusiano wa karibu kwa watoto wadogo, na namna uelewa wako unavyoathiri jinsi unavyofanya kazi katika masomo mengine:
  Mawasiliano na shughuli za kila.
  Kufanya kazi kwa kujenga uhusiano, n.k.

Utajifunza kuhusu Mwenendo wa Uhusiano wa karibu, Mwenendo wa Mlezi wa Msingi Salama Tabia ya Ugunduzi.

 

Malengo ya somo:

  • Lengo kuu la somo hili ni kuelewa umuhimu wa Nadharia ya Msingi ya Uhusiano wa karibu ili kuboresha kazi ya walezi na kulinda ukuaji salama wa watoto
.
  • Watoto bila kuwa na wazazi wenye msimamo wanakabiliwa sana na mabadiliko katika uhamaji wa walezi na ubadilishaji ambao unaweza kusababisha kutokuwa na ukaribu mzuri baadaye.
 Maendeleo ya mtoto kijamii na kihisia yanategemea sana uelewa wako wa jinsi mwenendo wa ukaribu wa mlezi ulivyo.

Katika masomo yanayofuata utafanyia kazi kukuza utendaji mzuri.