Somo la 4/19

Ukurasa wa 2/5: Mada A: Nadharia ya Msingi ya Uhusiano wa karibu na Mfumo wa Uhusiano wa karibu

Utangulizi wa Mada A: Nadharia ya Msingi ya Uhusiano wa karibu na Mfumo wa Uhusiano wa karibu

JOHN BOWLBY
John Bowlby alikuwa Mwingereza, mtaalamu wa magonjwa ya akili ya watoto ambaye alifanya utafiti wa hisia za huzuni kwa watoto ambao waliachwa na wazazi wao katikaVita vya Pili vya Dunia. Kutokana na uzoefu huo, aliunda Nadharia ya Uhusiano wa karibu kwa ukuaji wa mtoto wa binadamu.

Swali lake la kwanza lilikuwa: “Kwa nini watoto wanakuwa na uhusiano wa karibu na wazazi wao kwa muda mrefu baada ya kuzaliwa na wanapoendelea kukua?

KWANINI MAMALIA WOTE HUWA NA TABIA YA UHUSIANO WA KARIBU?
  • Katika mifumo ya maisha ya ujima “mama” (reptilia, samaki na wadudu) walikuwa na watoto wengi kwa wakati mmoja. Samaki mmoja wa rangi ya dhahabu aliweza kutaga maelfu ya mayai kwa saa moja. Lakini “mama” hajali kabisa watoto wake mara baada ya kutoka katika mayai. Hii ni kwa sababu “ukuaji wa mtoto” wa ubongo hukamilika wakati kijusi kikiwa bado ndani ya yai. Hivyo “mtoto” anapotoka nje ya yai, anakuwa tayari kupambana mara moja – anaweza kutambaa au kuogelea au kuwinda au kula papo hapo. Hahitaji “kutunzwa baada ya kuzaliwa” – ukuaji wa ubongo unakuwa umeshakamilika kabla ya kutotolewa.
  • Mamalia (wanyama wanaonyonyesha watoto wao kama vile: mbwa, paka, nyangumi, gorilla na binadamu) wana njia nyingine tofauti na ubongo ulio na mchanganyo zaidi. Wanakuwa na watoto wachache sana wanapokuwa wajawazito na wanatunza na kujali kila mtoto. Watoto wa binadamu wanazaliwa wakiwa na ubongo ambao haujakomaa na wazazi wanaweza kuunda na kuuprogramu ubongo kwa sababu unakuwa bado haujakomaa kwa miaka mingi. Watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa watu wazima namna ya kusoma, kufikiria, kushirikiana, kutatua matatizo n.k. Unajenga ubongo wako” kupitia ulezi na utunzaji kutoka kwa walezi.
  • Inachukua miaka 16 -17 kabla ubongo wa binadamu kukamilika, na katika miaka yote hiyo unahitaji matunzo na msaada kutoka kwa walezi
MASWALI
  • Je, una wanyama wa kufugwa au unamjua yeyote mwenye wanyama wa kufugwa? Je, wazazi wa wanyama hao wanawatunzaje watoto wao baada ya kuzaliwa?
  • Wanafanyaje wanapowatunza watoto wao? Wanawatunza kwa muda gani kabla ya kuwaacha wakajitegemee?
TABIA YA UHUSIANO WA KARIBU NI NINI?
  • Hakuna tatizo kubwa kwa mbinu hii ya ukuaji kwa wanyama: ubongo wa mtoto aliyezaliwa hauna uwezo wa kufanya kazi vizuri sana, hivyo watoto wanahitaji msaada – maisha yao yanategemea walezi watu wazima, hususan kwa miaka yao ya awali maishani.
  • Hii ndiyo sababu binadamu wana mfumo wa uhusiano wa karibu: kuhisi ukaribu kunampa mtoto usalama, ulinzi na matunzo. 
  • Hivyo tabia ya uhusiano wa karibu ni: Tabia ya mtoto mdogo kutafuta ulinzi, matunzo na kunyonyeshwa kutoka kwa wazazi au walezi.
  • Kama walezi wakimuacha mtoto, atakufa. Hivyo, watoto wanakuwa na tabia ya kuepuka kutenganishwa kimwili na wanaonyesha kwa kuwa na tabia ya kuwa karibu. Mfumo wa Uhusiano wa karibu unakuwa hai:
    • Mfumo wa Uhusiano wa karibu unachochewa na utenganishwaji na hata hofu ya kutengwa tu.
    • Kuepuka utenganishaji wa kimwili ni nafasi pekee ya mtoto kuishi.
    • Mtoto anaepuka kutenganishwa kwa kung’ang’ania, kulia, kumtafuta mlezi, kufadhaika na kuwa na huzuni, kujilinda wakati mlezi anapoondoka.
  • Hii ni kawaida na tabia ya uhusiano wa ukaribu kiafya. Watoto ambao hawaonyeshi hisia wakati walezi wanaondoka wanaweza kuwa wamekata tamaa ya kutafuta matunzo (kujitoa). Wanaweza kuelezwa kama “wakimya sana”, lakini tabia hii sio ya kawaida. Watoto ambao wanaonekana kuwa na hofu kubwa wakati walezi wanapoondoka wanaweza kukabiliwa na utengwaji mgumu na wa kutisha. Hizi sio hisia nzuri sana na mara nyingi zinaonekana kwa yatima ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kuwatunza.
MASWALI
  • Unaweza kufikiria jinsi utakavyowaona watoto wako wakionyesha tabia nzuri ya ukaribu – kulia unapoondoka au kung’ang’ania mtu au kitu, kupiga mayowe, kuwa na huzuni, n.k.?
  • Ni wakati gani unapoziona tabia hizi kwa watoto unaowatunza? Je, kuna watoto ambao hawaonyeshi hisia wakati walezi wanaondoka?
  • Je, tunafanya nini wakati watoto wanaonyesha tabia za kawaida za kuwa karibu?
  • Tunajibuje (kuwabembeleza, kuwakaripia, kufikiria kuwa ni “wasumbufu”, je tunapata usumbufu wanapolia? Au…?).
  • Je, wazazi watafanya nini katika utamaduni wetu wa asili wakati watoto wanaonyesha tabia ya kuwa karibu?
  • Je, mama yako alikueleza nini kuhusu jinsi ya kuwasaidia watoto wanaokung’ang’ania” …… babayako je?
ORODHA YA MAMBO YA KUELEWA
  • Nani alianzisha Nadharia ya Uhusiano wa karibu?
  • Kwa nini mamalia peke yao (hususan binadamu) wana mfumo wa uhusiano wa karibu?
  • Eleza tabia ya kawaida ya ukaribu kwa kutoa mfano wa kazi yako ya kila siku.
  • Waelezee watoto wenye tabia ya uhusiano mdogo wa karibu au wanaopata hofu ya kuwa na ukaribu katika kazi yako.
MAPENDEKEZO YA ZOEZI
Tumia kumbukumbu yako kukumbuka mazingira uliyoyaona, au simu yako, au kamera kurekodi tabia ya kawaida ya uhusiano wa karibu katika utaalamu wako wa matunzo ya mtoto kila siku. Je, watoto mbalimbali wanajisikiaje mlezi anapoondoka?