Somo la 4/19
Ukurasa wa 3/5: Utangulizi wa mada B: Kufanyia kazi Msingi Salama wa Mtoto ili kusaidia tabia ya ugunduziUtangulizi wa mada B: Kufanyia kazi Msingi Salama wa Mtoto ili kusaidia tabia ya ugunduzi
Kwa kuwa mfumo wa uhusiano wa karibu unafanya kazi, mtoto atatumia nguvu zake zote kumtafuta mlezi ili kuepuka kutenganishwa, na hii ni hali ya kuchosha sana kwa mtoto. Kwa upande mwingine watoto wote lazima wajifunze kuhusu utengenishwaji –walezi na wazazi wanapaswa kufanya mambo mengine pia. Unawafundishaje watoto kutoogopa sana wanapotenganishwa?
Mlezi anamfundisha mtoto jinsi ya kutengana bila hofu kwa kufanya mambo mawili:
- Mlezi anamfundisha mtoto kuhusu kutengana taratibu, hivyo mtoto hapati hofu.
Kwa mfano, mlezi anamlaza mtoto, anaondoka, mtoto analia, mlezi anarudi na kumbembeleza mtoto. Wakati mwingine utenganaji ni wa muda mrefu kidogo, na kadhalika. Unaweza kuona hili katika shule za awali (chekechea) asubuhi na wakati wowote mzazi atamuacha mtoto wake. Mwishoni mtoto hana hofu mama yake anapoondoka. Kama ataondoka ghafla au kwa kumkaripia na kuondoka mtoto ataendelea kulia na kuwa na hofu zaidi.
- Mlezi pia anamfundisha mtoto kumkumbuka mlezi anapokuwa hayupo karibu naye.
Kwa mfano, unaweza kuona mlezi akicheza titty-booh au mchezo wa kujificha na mtoto. Mlezi anamchekesha na kwenda nyuma ya mlango kwa muda mfupi na kuja mbele kabla mtoto hajaogopa sana. Kwa njia hii mtoto anajifunza kwamba “Yupo hata kama simuoni” Hii inamsaidia mtoto kujisikia salama hata kama mlezi ataondoka kwa muda.
Kama mlezi unaweza kuwa na mtoto/mtoto anayejifunza kutembea na kutumia njia hizo mbili za kumfundisha mtoto kuhusu kutenganishwa kwa utulivu.
Hapa ni mtunzaje wa mtoto anayejaribu kumfundisha mtoto mchezo wa
”peek a booh”