Somo la 6/19
Ukurasa wa 3/4 Mada B: Vipimo vya Mwenendo Salama wa MleziMada B: Vipimo vya Mwenendo Salama wa Mlezi
Haihusu sana kile unachofanya (kazi), bali namna unavyofanya (ubora wa uhusiano). Namna unavyohusiana na mtoto (hususani miaka miwili ya mwanzo ya maisha) ni mchakato wa kujifunza, ambapo mtoto hujifunza namna ya kukabiliana na kutenganishwa na namna ya kuhusiana na watu wengine. Anajifunza hili kutoka kwa mlezi wa kwanza, na mwingiliano na walezi wa awali hujenga Mwelekeo wa uhusiano wa karibu na mtoto.
Walezi hutekeleza Utaraibu wa Ukaribu ulio Salama
Atatafuta huduma na msaada wakati anapohitaji. Si tu kwamba ataweza kucheza na watoto wa rika lake, bali pia ataweza kumuacha rafiki na kuwatafuta wengine wa kucheza naye anapochoshwa na baadhi ya mchezo. Atapendelea baadhi ya walezi kuliko wengine kwa sababu anajisikia kuwa nao karibu zaidi kuliko wengine, na atawapendelea baadhi ya watoto wa rika lake kuliko wengine na kuanzisha urafiki nao. Mtoto anapokua mkubwa, atafanya vizuri katika uhusiano wa kijamii, na ataweza kujifunza kwa kadri inavyowezekana shuleni na kwenye taasisi nyingine.
Hii inatokea iwapo tu walezi wanahusiana na mtoto kwa njia salama.
MAWASILIANO YA PANDE MBILI:
Walezi wanafanya nini kumpa mtoto uhusiano salama na kujenga utaratibu wa ukaribu ulio salama kwa mtoto:
Mara nyingi huitika pale mtoto anapotaka mawasiliano. Pia, mara nyingi hufanya juhudi kuwasiliana na kumchangamsha mtoto. Wanatumia sauti za tuni nzuri na mwonekano wa uso wenye tabasamu ili kuonyesha jinsi wanavyojisikia. Wanaongea na mtoto na kujaribu kumwangalia machoni.
Video hii inaonyesha mwelekeo ambao unaitwa mawasiliano ya pande zote kwa njia tatu mbalimbali. Maana ya mawasiliano ya pande zote ni kuwa msikivu katika mawasiliano pamoja na mtoto mchanga au pamoja na mtoto. Kwanza na mtoto mchanga, gundua jinsi mlezi anavyofanya mawasiliano ya macho na kutumia sauti nzuri ya kupendeza wakati anambembeleza mtoto mchanga ili mtoto atulie na ajisikie salama. Pili na mtoto mdogo: Gundua jinisi shughuli ina ridhimu. Tatu mlezi anapanga mpango wa chakula pamoja na wavulana: Kitu cha muhimi hapa ni kwamba mlezi anasikiliza na anawapa kipaumbele juu ya nini wavulana wanasema. Maneno mengine muhimu ni kuwashirikisha katika mazungumso.
KUWA MAKINI:
Walezi wanafanya nini kumpa mtoto uhusiano salama na kujenga utaratibu wa ukaribu ulio salama:
Hutenda kwa namna inayojenga hisia. Wana kazi za (kumlisha mtoto, kumvalisha nguo, kumwimbia nyimbo au kufanya shughuli nyingine, n.k.), lakini “husoma” hisia za mtoto na kutatua tatizo hilo kwa njia mwafaka: kama mtoto ana masikitiko, wanamliwaza mtoto wakati wanamvalisha viatu, kama mtoto ana furaha kuvaa viatu kutakuwa ni mchezo, n.k. Kuwa na hisia kunamaanisha kwamba huhitaji kufuata sheria kali, unammotisha mtoto kwa ” kukutana na kuelewa namna mtoto anavyojisikia sasa.
Angalia hii video jinsi mtoto anavyoshindwa kumaliza kazi yake ya shule. Mlezi anasoma jinsi mtoto anavyojisikia, halfu mlezi anavyomsoma mtoto na kumuelewa mtoto. Angalia jinsi mlezi anvyokutana na mtoto na kumuelewa mtoto.
UWEPO MTOTO ANAPOKUHITAJI:
Walezi wanafanya nini kumpa mtoto uhusiano salama na kujenga utaratibu wa ukaribu ulio salama:
Wanapatikana kwa ajili ya watoto. Kama mtoto ana msongo, masikitiko, au ana uhitaji, kuna mlezi karibu kwa ajili ya kumliwaza na kubelembeleza, kutoa msingi salama. Huduma hutolewa bila masharti na kwa haraka, mpaka mtoto ajisikie salama tena.
Kwenye mfano huu kutoka Tanzania wakina mama wanaonesha kwa watoto uwepo wao, watoto wanapowahitaji wakina mama kwa msaada wao.
PATA HISIA ALIZO NAZO MTOTO, LAKINI SI KWA NAMNA ILIVYO KWA MTOTO:
Kama mtoto ana hasira, huzuni au amekata tamaa, mlezi hupata hisia hizo za mtoto lakini si kama mtoto huyo. Hata kama mtoto ana mshutuko au hasira, mlezi hapaswi kushtuka au kuwa na hasira – hubakia katika hali ya utulivu. Mlezi hapaswi kumkemea au kumwadhibu mtoto. Anaweza kuwa imara lakini hajisikii hasira kama mtoto anavyojisikia, na anazungumza na mtoto kwa njia ya huruma na utulivu. Mtoto atakuwa hayuko salama kama mlezi pia atakuwa na hasira pale mtoto anapokuwa na hasira.
Angalia kwenye mfano huo jinsi mtunzaji wa mtoto mdogo wa kike anavyokuwa mtaratibu japokuwa mtoto anachanganyikiwa na externalising.
Anamsaidia mtoto aweze kugundua hisia zake bila kumsema mtoto wala mama mwenyewe kuchanganyikiwa. Anaelewa hisia za mtoto bila kumonyesha mtoto kwamba kitu anachofanya ni sahihi na mtoto anaendelea kucheza.
MENTALIZING: KUTAFAKARI MAWAZO NA HISIA ZA MTOTO:
Walezi wanavutiwa na kile ambacho mtoto anahisi na kufikiria, na wanajaribu kuakisi hali ya hisia na fikra za mtoto. Hata kabla mtoto hajaweza kuelewa maneno, wanaongea na mtoto wakati wanashughulikia kile ambacho mtoto anahisi au kufikiri.
Video hii inaonyesha mlezi anavotumia mbinu ya mentalizing. Mlezi anamsikiliza mtoto na anamsaidia kutambua hali na hisia yake. Kwa kumwambia kwamba ni sawa kupoteza kitabu na kwamba kila kitu kitakuwa sawa, mlezi anaonyesha upendo juu ya jinsi mtoto anavyojisikia na kumpa uweleo juu ya hali yake.
Kama ukiangalia kazi zako za kawaida za kila siku na mtoto: Ni kazi zipi unazoweza kuzipa uzingativu zaidi kuwaitikia watoto pale wanapotaka mawasiliano?
- Mawasiliano ya pande mbili: Je, una kazi za kila siku ambazo unazipa uzito zaidi kwa mawasiliano ya pande mbili kati ya mlezi na watoto wengine (kuimba, kucheza, n.k.)? Unawezaje kufanya shughuli za mawasiliano ya pande mbili na watoto wakati ukifanya kazi zako za vitendo?
- Kuwa makini: Fikiria kazi za kila siku na fikiria namna mtoto mmoja mahususi anavyotoa mwitikio kwa kitu ambacho anapaswa kufanya (kula, kuvaa, n.k.) Ni njia gani nzuri ya kummotisha mtoto huyu kufanya kazi hii? Je, unawezaje kuwa makini kwa mtoto huyu– ni tabia gani ya mlezi inaweza kuleta matokeo mazuri zaidi?
- Uwepo mtoto anapokuhitaji: Kama mtoto anahitaji uzingativu au msaada wetu (anaogopa, hayuko salama, hana furaha, ana maumivu) anapaswa kusubiri kwa muda gani kabla hatujamsaidia? Hakuna mahitaji kutoka kwa mlezi kuhusu namna ya kufanya ili kupata msaada, unapata kama unauhitaji. Kama kuna watoto wengi na walezi wachache, tunaweza kufanya nini kutatua tatizo hili, ili tuwepo wakati watoto wanapotuhitaji?
- Pata hisia alizo nazo mtoto, lakini si kwa namna ilivyo kwa mtoto: Pale mtoto anapokuwa hana raha, ana hasira, muda wote anabisha, anasumbua au anahamaki kwa hasira: Ni kwa namna gani hisia za mtoto zinavyotuathiri na kutufanya tutoe mwitikio? Ni kwa namna gani tunaweza kutoa uzingativu kwa kile kinachotutokea, na kuwa watulivu, imara na wapole hata kama mtoto hana sababu ya msingi au amekuwa na mshtuko zaidi? Ni kwa vipi watoto wanaweza kutufanya tukasirike au tuudhike? Ni kwa namna gani tunaweza kutoa uzingativu maalumu tusijisikie kama hao watoto? Ukiakisi mawazo na hisia za mtoto: Ni kwa namna gani tunaweza kuzungumza na watoto wakati tunawahudumia?
- Mentalizing: Kutafakari mawazo na hisia za mtoto: Ni jinsi gani tunaweza kuongea na watoto juu ya mawazo yao na hisia zao, na kuwafundisha ni jinsi gani watu wengine wanajisikia. Kwa mfano: Pale tunapofanya kazi na mtoto, pia tunazungumzia kile tunachoona kinatokea kwa mtoto: “Sasa unaenda kucheza na mdoli huu – ninaweza kuona unamuogopa kidogo kwa sababu hujawahi kumuona kabla- Ni vizuri, hebu tumuangalie kwa pamoja” au “Sasa unakunywa kutoka kwenye chupa yako, Kweli una njaa, ni vizuri sana kula, ambako kutakufanya ufurahi, au sivyo?” nk.
- Fikiria ni kwa vipi unaweza kuboresha namna unavyohusiana na watoto (mawasiliano ya pande mbili, kujenga hisia, n.k.).
- Tafuta mifano ya kila siku na tafakari namna unavyoweza kujenga uhusiano.
- Tafakari kuhusu ni matatizo gani hasa yanayoweza kuwepo katika kuboresha uhusiano (“Nina kazi nyingi, Ni vigumu kufanya kitu kipya, kuna watoto wengi na ni mimi tu”, nk. ) na tafakari ni kwa namna gani unaweza kuyaondoa matatizo hayo.
- Tafakari namna ambavyo mitazamo hasi ya nyuma inaweza kuzuia tabia ya kutoa huduma salama
-
- “Wazazi wangu mara zote walinikemea, nitajizuiaje kufanya hivyo ninapofanya kazi?”
- “Kama mlezi hupaswi kuwa na uhusiano binafsi na watoto”
- “Hatuna muda wala nguvu ya kufanya yote haya”
- ” Kama watoto wanaanza kujenga uhusiano wa karibu na mimi, watakuwa na huzuni nitakapoondoka nami nitahuzunika”
Mitazamo yote hii ina ukweli ndani yake, hata hivyo unapaswa kuiacha, si mizuri kwa makuzi ya mtoto. Ndiyo, kama hukupata malezi mazuri kutoka kwa wazazi wako unapaswa kuwa mlezi unayetoa huduma nzuri, lakini unaweza kufanya hivyo.
Kuwa na uhusiano binafsi na watoto na kuwafanya wawe na uhusiano wa karibu na wewe kwa hakika ni sehemu muhimu sana ya kazi ya mlezi.. Ndiyo, watoto watahuzunika utakapoondoka kama unawaruhusu kuwa na uhusiano wa karibu nawe, lakini hii ni sehemu ya maisha ni vizuri zaidi kwao kuliko kama wasingejifunza kabisa kuwa na uhusiano binafsi na mlezi.
Uhusiano wa karibu unafaa sana kwa mtoto yeyote.
- “Labda tunapaswa kugawa kazi yetu ili tuwe na kazi sana kwa muda fulani na tusipatikane sana, na muda mwingine wakati wa mchana tutawaonyesha watoto kwamba sasa tunapatikana sana na tuna muda wa kuwapa uzingativu.”
- “Tuna watoto wengi kwa mlezi mmoja, kwa hiyo muda mwingine tunaamua kuwa nao pamoja katika makundi, wakati mwingine tunawahudumia mmoja baada ya mwingine. Kwa mfano, kila mchana tunafanya kazi ambayo tunamhudumia mtoto mmoja baada ya mwingine wakati watoto wengine wakiangalia.”