Somo la 9/19
Ukurasa wa 3/10 Utaratibu usio salama wa uhusiano wa karibu kwa watoto (ukwepaji, ukinzani na kutokuwa na utaratibu mzuri) na tabia za waleziUtaratibu usio salama wa Uhusiano wa karibu kwa watoto (ukwepaji, ukinzani na kutokuwa na utaratibu mzuri) na tabia za walezi
Unakumbuka kutoka katika somo la 6 namna watoto wanavyofanya wanapopata matunzo salama katika miaka yao ya mwanzo ya maisha:
- Walezi wanapotoa msingi salama, mtoto wa miaka 0-2 huwa na huzuni wakati mlezi anapoondoka – lakini sio kwa muda mrefu. Mara ataanza kuondoka kwa kutambaa na kutumia muda mwingi kwa kucheza na kuchunguza.
- Watoto wakubwa mara nyingi watajitegemea na kuwa na maoni chanya kuhusu wao wenyewe na wengine, na watatafuta msaada utakapohitajika. Watakuwa na uhusiano maalumu na wanarika wenzao pamoja na walezi.
Kuna utaratibu mwingine wa tatu ambao unaonyesha uhusiano salama na walezi wa kwanza. Tafadhali wafikirie watoto waliopo katika matunzo yako wakati tunaendelea kujifunza utaratibu wa uhusiano wa karibu usio salama. Baada ya ufafanuzi tutafafanua namna watoto waliopo katika matunzo yako wanavyoonyesha hisia unapoondoka, au unapokuwa na uhusiano nao.