Somo la 9/19
Ukurasa wa 5/10 Tabia isiyo salama ya kuepuka uhusiano wa karibuTabia isiyo salama ya kuepuka uhusiano wa karibu
Kama mtoto au mtoto mdogo atakutana na walezi ambao hawapatikani sana, ambao wana mambo mengi ya kufanya na hawaonyeshi upendo mkubwa kwa mtoto, anaweza kuonyesha hisia zake kwa kujenga mtindo wa kumuepuka mlezi na watu wengine muhimu. Anaweza kujaribu “kujifanya amekua kidogo” au “kuwa mzazi yeye mwenyewe”.
- Mtoto hawezi kuonyesha hisia kwa kulia wala kuwa na huzuni wakati mlezi anapoondoka.
- Atakuwa akitumia muda wake mwingi kucheza na midoli au kufanya shughuli nyingine, na hatawasiliana na mlezi anaporejea. Anakuwa na tabia ya kupuuza matunzo yake.
- Watoto wakubwa na vijana: hawataomba msaada au huduma hata kama wanahitaji.
- Watajaribu kudhibiti hisia zao, na hawataonyesha kwa uwazi wanavyojisikia.
- Watajaribu kutatua matatizo yao wao wenyewe mapema kadri wanavyokua.
- Watakuwa wakikumbuka matatizo na kuzungumza kuhusu matukio ya huzuni au mamatatizo kama vile kutengana na kupoteza wazazi.
- Watathamini kuwa huru na kutoonyesha au kuzungumzia kuhusu hisia zao.
- Mara nyingi wataonekana wakiwa na dharau, wenye mawazo mengi, wenye hisia kali na wanasema mambo kama “Nani anajali?”, “Huwezi kuwaamini watu wazima”, n.k. Kwa kawaida wanakuwa katika hali ya “kukaa peke yao”.
- Mara nyingi wanaonekana wakiwa peke yao na wenye huzuni, lakini hawataki kuzungumzia hali hiyo.
Watoto wenye mbinu hiyo ya kuepuka hujaribu kukabiliana na kupoteza wazazi na kukosa huduma kwa kuacha kutafuta huduma na badala yake hujenga ukaribu zaidi na vitu (kama vile midoli au kufanya shughuli mbalimbali) badala ya watu kujenga hisia za usalama. Kimsingi watoto wenye tabia ya ukwepaji, wana uhitaji mkubwa wa matunzo, lakini wamejifunza namna ya kuyaficha kwa sababu mlezi wa kwanza alikuwa na kazi nyingi za kufanya, hakujali hisia na alikuwa hapatikani. Hii inamaanisha kwamba mara nyingi wanaeleweka kama “baridi”, na waliosahaulika kwa kazi za kila siku kwa sababu hawahitaji uzingativu wala msaada wa mlezi.
MATUNZO YA KITAALAMU DHIDI YA WATOTO WANAOJITENGA
Kwa watoto wenye tabia ya kuepuka matunzo, baadhi ya vipengele vya usalama wa walezi ni muhimu:
- Mjali mtoto kila unapomuona kuwa anahitaji – chukua jitihada za kujali hata kama mtoto hakuomba au anataka kukaa peke yake.
- Muonyeshe kwamba wakati wote unapatikana na upo tayari kumzingatia au kuzungumza na mtoto.
- Onyesha hisia zako zikiwa tayari na “tafsiri” unachodhani mtoto anaweza kuhisi kupitia maneno yako. Kwa mfano.: “Oh mpendwa, unalala kwenye sakafu –hiyo itakuumiza sana – njoo ukae na mimi kwa muda”.
- Sisitiza taratibu na kwa upole – mtoto anakuhitaji, lakini anaogopa kukuonyesha mahitaji yake.
- Tumia kugusana kusiko kw amoja kwa moja: inaweza kuwa ngumu sana kwa mtoto anayejitenga kuzungumzia mambo yake binafsi, lakini mara nyingi anaweza kupenda sana vitu na kuwa karibu sana navyo. Hivyo kwa mfano unaweza kutafuta kitu anachokipenda sana kama vile mdoli wa mtoto au mchoro na kuzungumza na mtoto kuhusu jinsi “ mdoli anavyojisikia” au vitu vilivyopo katika mchoro vinafanya nini, vinafikiria nini au vinajisikiaje. Kisha mtoto atazungumza kuhusu yeye mwenyewe “kupitia kitu” ulichomshirikisha.
TAFAKARI
- Je, unamuona mtoto yeyote unayemlea akifanya hivyo?
- Unafanya nini wanapoepuka mawazo, matakwa na utambuzi wa mlezi?
- Je, unamkumbuka mtu yeyote katika familia/marafiki zako anayefanya kama hivi?
- Kuna ugumu gani kwako katika kukabiliana na hali wakati watoto wanapokuwa na tabia ya kujitenga?