Somo la 9/19
Ukurasa wa 10/10 Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuataMpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata
“Walezi wote wana shauku ya kushirikishana matokeo ya utekelezaji wao (…). Kwa mfano wanashirikishana jinsi mtoto mmoja ambaye amekuwa hatabasamu sasa ameanza kutabasamu tangu mlezi wake alipoanza kutumia mwelekeo wa uhusiano ulio salama wa matunzo na yeye. Alieleza jinsi alivyoweza kupatikana na kuwa makini kwake wakati akiwa mkali kwake kwa sababu ya tabia yake ya ukinzani”
Kauli ya mwalimu
ORODHA YA MAMBO YA KUELEWA
- Nini kinachosababisha tabia ya ukaribu usio salama kwa mtoto?
- Unaitambuaje tabia ya kuepuka kujenga uhusiano wa karibu?
- Utatatuaje kitaalamu dhidi ya tabia mtoto ya kujitenga?
- Utaitambuaje tabia ya ukinzani katika uhusiano wa karibu?
- Utatatuaje kitaalamu dhidi ya tabia ya ukinzani kwa mtoto?
- Utaitambuaje tabia ya kutofuata utaratibu katika kujenga uhusiano wa karibu?
- Utatatuaje kitaalamu dhidi ya tabia ya kutofuata utaratibu kwa mtoto?
- Ni wakati gani katika maisha ya mtoto unapopata nafasi nzuri ya kumsaidia kujenga uhusiano salama wa karibu?
MAMBO YA KUFANYA KABLA YA SOMO LINALOFUATA
Tafadhali zingatia:
- Mtoto wako anaonekana kuonyesha mikakati gani? Hili liko wazi zaidi mwanzoni mwa uhusiano na wazazi walezi, au katika mazingira au kila siku ambapo mtoto anahisi hayuko salama, kuzongwa au kuogopa.
- Fikiria mazingira ya kila siku ambapo mtoto anaonyesha mashaka. Panga utakavyolishughulikia hili na tabia ya usalama ya mlezi:
- Kuwa mtulivu, mwepesi kuhisi, mkarimu na thabiti wakati mtoto anapokukataa au kukulaumu.
- Unawezaje kumpa mtoto msaada hata kama haonyeshi kama anahitaji msaada? Utaonyeshaje hisia zako kwa uwazi?
- Je, mbinu za uhusiano wa karibu za mtoto zimebadilika wakati wote wa uhusiano na wazazi walezi? Je, mtoto anaweza kukabili kujikana kabla ya kurejea katika utaratibu wa zamani kama vile kutoamini au kukosekana kwa imani katika ukweli kwamba mtu fulani ataweza kumsaidia? Je, mtoto anaeleza mitazamo chanya ya kwake au ya uhusiano wake kwa kiwango kikubwa?
ZOEZI
Muelezee mtoto aliye katika malezi yako katika uhusiano mwingi wa kila siku ukionyesha ama:
- Kujitenga
- Ukinzani
- Tabia ya kutofuata utaratibu
Rejea katika mwitikio wako kwa tabia ya mashaka ya mtoto.Ni wakati gani ni vigumu kutenda kwa usalama? Ni wakati mtoto anapokukasirisha, anakukwepa, anakukaripia, anakupuuza au mambo mengine?
Asante kwa utayari wako na kila la heri katika kazi yako hadi somo linalofuata!