Somo la 12/19
Ukurasa wa 2/3 Majukumu na Uhusiano katika ushirikiano na mwajiri wakoMajukumu na Uhusiano katika ushirikiano na mwajiri wako
Kama ilivyoelezwa katika Kadi ya maelezo kutoka mwanzoni mwa programu hii, matokeo ya ulezi yanategemea sana mtandao wako wa kijamii, na sehemu muhimu sana ya jambo hili ni uhusiano na mamlaka zilizokuajiri kama familia mlezi.
Mada A: Kushirikiana na Mfanyakazi wa Huduma za Jamii
Wafanyakazi wa huduma za jamii wanawajibika kufafanua matatizo na mahitaji ya mtoto kwa kushirikiana na wazazi, kwa ajili ya kuchagua aina ya mahali pa kuishi, na kwa ajili ya kuandaa mpango wa muda mrefu wa mahali pa kuishi. Kazi hizi zote zimeelezwa katika Sheria ya nchi yako.
Wafanyakazi wa huduma za jamii na familia walezi huangalia mahali pa kuishi kwa namna tofauti. Wafanyakazi wa huduma za jamii wana jukumu la kuangalia familia asili kwa ujumla wake, na mara nyingi wanalenga haki na mahitaji ya wazazi halisi.
Wafanyakazi wa huduma za jamii pia wanabanwa na Sheria na uamuzi wa mahakama (kama vile mahakama kuamua kwamba mtoto anapaswa kurejeshwa katika familia halisi).
Malezi yako ni moja ya matukio mengi, ambayo anapaswa kusimamia na wakati mwingine muda wa kuwasiliana nawe unaweza kuwa mdogo kutokana na idadi kubwa ya matukio. Changamoto nyingine inaweza kuwa eneo lake la kazi linaweza kuwa halina mpangilio mzuri na kwamba mfanyakazi wa huduma za jamii anaweza kubadilisha kazi au nafasi. Hili linaweza kuleta ugumu kwa mamlaka kujenga uhusiano unaofaa wa muda mrefu na wazazi walezi.
Wazazi walezi huangalia mahali pa kuishi kwa namna tofauti – bila shaka wako karibu zaidi na mtoto, wanajua hisia na matatizo ya mtoto na kujenga ukaribu wa kihisia na mtoto.
Hili linaweka wazi kwamba nafasi hizo mbili zinaweza kutoa mawazo mawili tofauti kabisa kuhusu nini kinawezekana na ni nini kinafaa “kwa matakwa mazuri ya mtoto”. Kazi ya kitaalamu ya wazazi walezi ni kuelewa tofauti kati ya nafasi hizi mbili na si kuziangalia kama suala binafsi.
Hili katika matukio mengine linaweza kuwa linatoa changamoto kubwa, lakini utafiti unaonyesha kwamba ukuaji mzuri wa mtoto unatokana na uhusiano mzuri na uelewa kati ya mfanyakazi wa huduma za jamii na wazazi walezi.

MAPENDEKEZO KWA AJILI YA KUUNDA USHIRIKIANO NA MFANYAKAZI WA HUDUMA ZA JAMII
- Mwambie mfanyakazi wa huduma za jamii akupe karatasi inayoelezea kazi zako na malengo muhimu sana katika kazi yako kwa mtoto anayelelewa. Karatasi hiyo itarahisisha kwa mfanyakazi wa huduma za jamii anayefuata kama kutakuwa na mabadiliko ya mtu unayefanya naye kazi.
- Mpe mfanyakazi wa huduma za jamii nakala ya Kadi ya maelezo na vitini vyako muhimu zaidi. Hii itampa uelewa wa nini ulichogundua kuwa muhimu mahali mtoto alipowekwa kuishi.
- Mwambie mafanyakzi wa huduma za jamii aina ya mawasiliano (na mara ngapi) mnatarajia kukutana wakati mtoto akiwa katika ulezi wako.
MADA ZA KUTAFAKARI
- Je, ulikuwa na mkutano wa kwanza na mfanyakazi wa huduma za jamii, ambao ulikupa uelewa bayana wa mkataba wako, aina ya kazi, na nini ambacho mamlaka zinachukulia kuwa matokeo mazuri ya kazi yako.
- Umezungumza mara ngapi na mfanyakazi wa huduma za jamii na je mazungumzo yako yalisbabisha makubaliano na ushirikiano?
- Je, mfanyakzi wa huduma za jamii alifafanua ni mara ngapi mtoto anapaswa kukutana na wazazi wake halisi, na hili linafanyikaje?
Mada B: Ushirikiano na walimu na/au meneja kutoka katika asasi ya familia mlezi
Kwa baadhi ya nchi kitengo cha huduma za jamii hutoa mafunzo na usimamizi kwa wazazi walezi. Wakati mwingine pia husimamia mkataba unaohusu mahali pa kuishi mtoto. Hili linashughulikiwa na mameneja na/au wasimamizi wa wazazi walezi. Kazi ya watu hawa ni: kukusaidia katika kujenga uhusiano wa kitaalamu na mtoto, kutafakari na wewe kuhusu matatizo magumu na masuluhisho katika maisha ya kila siku, na kujadili namna ya kutenda na kupanga katika kazi zako za kila siku na mtoto.
Kwa sababu kazi zao ni kusaidia kazi zako na kwa sababu wanafanya kazi kwa karibu sana na wazazi walezi, bila shaka watakuwa wanajua zaidi namna unavyoona huduma ya ulezi. Hii inamaanisha kwamba unapaswa kujaribu kuwa mwelewa wa mawazo ya wengine na kuyakubali kadri inavyowezekana na pia eleza changamoto binafsi sana unazoweza kupitia katika kazi yako kama wazazi walezi.

MAPENDEKEZO KWA AJILI YA KUJENGA UHUSIANO MZURI NA MSIMAMIZI/MENEJA
- Kabla hujatembelewa na mtu, fikiria au andika kuhusu orodha fupi ya mambo muhimu sana unayotaka kuzungumzia. Kama inawezekana, itume kwa mtu huyo kabla ya kukutana.
- Kama utaona ni vigumu kuzungumzia matatizo binafsi yanayokuathiri, mwambie mtu huyo jambo hilo. Wakati mkiwa wazazi walezi, inaweza kuwa muhimu kuzungumza kuhusu hisia binafsi, kwa sababu mwitikio wako binafsi kwa sasa ni sehemu ya kazi yako ya utaalamu. Hivyo wewe na msimamizi ni lazima msaidiane kutafuta kikomo kati ya nini ni binafsi na nini lazima kijadiliwe kwa sababu kinaathiri njia yako ya kitaalamu ya kutoa huduma.
- Kazi ya kumlea mtoto inaweza kuwa ngumu sana, na wakati mwingine unaweza kukata tamaa na mfumo unaopaswa kukusaidia, au kutokukubaliana na uamuzi uliotolewa. Tunapendekeza kwamba mwambie msimamizi jambo hili iwapo litatokea, lakini pia dumisha mtazamo halisi na kubali ushauri licha ya matatizo hayo. Migogoro kati ya wazazi walezi na mamlaka au wasimamizi kamwe haimfaidishi mtoto katika maisha yake. Hata hivyo, unapaswa wakati wote kutumia njia nzuri kusisitiza hilo ili kupata msaada unaohitaji kutekeleza kazi yako.
MADA ZA YA KUTAFAKARI KAMA UNA MSIMAMIZI
- Unajisikiaje kumwambia mtu changamoto ngumu katika uhusiano na mtoto au na wazazi wake?
- Unajisikiaje kuzungumzia changamoto zako binafsi katika kufanya kazi na mtoto au matatizo ya ndoa katika familia mlezi, ambayo yanaweza kuathiri uhusiano wa huduma za ulezi na mtoto huyo?