Somo la 11/19

Ukurasa wa 2/4 Kuwa na vyanzo vingi vya kukuza utambulisho

Kuwa na vyanzo vingi vya kukuza utambulisho

Mara nyingi inakanganya kwa watoto waliowekwa mbali na nyumbani kwao kujisikia kuwa karibu na watu mbalimbali na wenye asili ya utamaduni tofauti. Mara nyingi sana ukaribu wao huvunjika ghafla katika hali ambayo mtoto anaweza kuwa aliogopa sana. Kwa mfano mtoto anaweza kuwa ameondolewa kwa nguvu na mamlaka wakati wazazi wamekata tamaa na kuwa na hasira, au mzazi anaweza kuwa amefariki au kukasirika wakati utengano ulipotokea.
Uzoefu huo wa utotoni hufanya iwe vigumu zaidi kwa watoto kujenga wazo ambalo ni wazi kuhusu wao ni nani na kwao ni wapi. Watoto wanajibainisha na wazazi wao na mara nyingi wanajenga mawazo hasi au ya kukanganya kuwahusu wao wenyewe kama hawatapata msaada. Matatizo hayo ni yapi na unawasaidiaje watoto kujenga mawazo chanya wenyewe wakiwa kwenye ulezi?
KUWA KATIKA FAMILIA MBILI: MIGOGORO YA UTII NA UTAMBULISHO

Angalia video hii juu ya mazungumzo kati ya mlezi na kijana. Kijana ana wasiwasi wa kuwatembelea ndugu zake. Angalia jinsi mlezi anavyomsikiliza kwa makini msichana na jinsi anavyomuelewa hisia zake. Katika mazungumzo mlezi anakuwa anamsaidia vizuri sana msichana kuweza kukabiliana na wasiwasi na kumfanya anaweza kutabasamu.

Mtoto – hususani kama ni mkubwa kuzidi miaka mitatu pale anapopata ulezi–tayari ameshajenga uhusiano wa karibu kwa wazazi. Kutokana na mtazamo wetu uhusiano huo wa karibu unaweza usifanye kazi na kujaa woga mwingi na hisia kinzani, Wazazi wanaweza kushindwa kutoa matunzo mazuri, lakini hata hivyo uhusiano huu wa karibu ni sehemu muhimu ya utambulisho wa mtoto.

Wanapowekwa kwenye familia mlezi, mtoto mara nyingi anakutana na mgogoro wa utii: ” Niko karibu na wazazi wangu – lakini wazazi walezi wangu wananijali na kunipenda. Ninawezaje kulipokea hili bila kujisikia hatia au kama msaliti kwa wazazi wangu?”

Mgogoro huu alio nao mtoto unaweza hata kuwa na maumivu zaidi kama wazazi wake wana masuala ambayo hayajatatuliwa ( hasira, wivu) dhidi ya familia mlezi, kwa kuwaona kama mtu aliyeiba moyo wa mtoto wao. Ni vigumu kuamua wengine wamhudumie mtoto wako na vigumu zaidi kama “familia mpya” ina mali zaidi.

MWITIKIO WA KWANZA WA WAZAZI WALEZI NA WAZAZI HALISI
Kama ukipokea mtoto kwenye malezi ambaye amekumbana na vurugu au kutelekezwa ni kawaida kuwa na hisia za ukatili na hasira dhidi ya wazazi ambao wanaweza kuwa wamemuacha mtoto katika matukio ya kutisha, au ambao hawawezi kutimiza ahadi kwa ajili ya kumtembelea na kukutana na mtoto wao. Mwitikio mwingine wa asili ni kuwa na mtazamo huu, “Tusahau yote kuhusu wazazi wako na ujisikie salama ukiwa na sisi”. Hili linaweza kuwa wazo zuri kwa mara ya kwanza hadi pale mtoto ametulia kwenye familia mlezi na kujisikia salama. Baada ya kipindi hiki, anzisha mazungumzo kuhusu kuwa na jozi mbili za familia ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza utambulisho.

Kama ilivyoelezwa kwenye masomo mengine watoto wadogo sana huweza kujenga uhusiano wa karibu na wazazi walezi baada ya muda fulani. Kama hii ikitokea, yamkini mtoto ataanza kukuita “mama” au “baba”. Unaweza kukubali hili ukijua kwamba mtoto atakapokuwa mkubwa atatafuta namna ya kuelewa historia yake mwenyewe. Labda mtoto mdogo au mtoto anayejifunza kutembea atakuchukulia kama mzazi. Lakini lazima ajifunze akiwa na umri mdogo kuelewa kwamba pia ana wazazi halisi. Katika umri wa miaka mitatu au minne kwa kawaida unaweza kuanza kuzungumzia “una jozi mbili za wazazi” Hii inapaswa kufanyika kabla mtoto hajasikia kutoka kwa watoto wengine au watu wazima kwamba ninyi si ” wazazi halisi”.

Hizi hisia asili za wazazi walezi kwa wazazi halisi lazima zitatuliwe – na hii huchukua muda – ili kwamba isimuweke mtoto anayelelewa katika mgogoro mkubwa wa kugawa utii. Ni muhimu kuelewa kwamba hasira au chuki yoyote kwa wazazi itachukuliwa na mtoto kama hasira kwa sehemu ya utambulisho wa mtoto mwenyewe.

Mtoto anayelelewa anaweza kwa hiyari yake kukana au kujaribu kuwasahau wazazi wake, lakini gharama ya hili itakuwa kwamba atagawanyika mwenyewe kwa sehemu moja kuwa na uhusiano wa karibu na wazazi wake na sehemu nyingine uhusiano wa karibu na wazazi walezi, bila kuweza kuwaunganisha hawa wawili kuwa wamoja katika dhana moja iliyo wazi. Hatimaye, hili litakuwa tatizo kwa mtoto, hususani katika umri wa ujana balehe wakati kijana anajaribu kujenga utambulisho wa utu uzima. Kila mara mtoto anapofikia hali mpya ya kukua kisaikolojia na kupata uelewa uliopevuka zaidi kumhusu yeye mwenyewe, lazima ajenge wazo jipya kuhusu utambulisho na historia, hivyo ni mchakato ambao unachukua miaka mingi.

KUONYESHA HESHIMA KWA MTOTO KWA KUWAHESHIMU WAZAZI WAKE
Tafiti zinaonyesha kwamba migogoro kati ya wazazi asili na wazazi walezi ina madhara katika kukua kwa mtoto – bila kujali migogoro inahusu nini.

Mitazamo yako kwa wazazi pia ni ujumbe kwa mtoto kuhusu kama anaweza kujiheshimu na kujisikia fahari ya yeye ni nani – mitazamo hasi kwa wazazi itazalisha kujiamini kusiko kuzuri kwa mtoto. Moja ya kazi ngumu kwa mzazi mlezi ni kukuza mtazamo chanya wa kweli wa wazazi ili kumsaidia mtoto.

MWASWALI YA KUTAFAKARI NA MAZUNGUMZO
  • Ulipompokea mtoto, ulijisikiaje kuhusiana na wazazi wake?
  • Uliona matatizo gani kwa mtoto ambayo yalisababishwa na kukosa ulezi wa wazazi?
  • Ulimwelezaje mtoto kuhusu namna unavyowaona wazazi wake?
  • Mtoto alikuwa anaelewa nini kuhusu kuwa kwenye ulezi?
  • Ni kitu gani kigumu sana kwako katika kuwakubali wazazi au kuona sifa zao nzuri?