Somo la 11/19
Ukurasa wa 2/4 Kuwa na vyanzo vingi vya kukuza utambulishoKuwa na vyanzo vingi vya kukuza utambulisho
Uzoefu huo wa utotoni hufanya iwe vigumu zaidi kwa watoto kujenga wazo ambalo ni wazi kuhusu wao ni nani na kwao ni wapi. Watoto wanajibainisha na wazazi wao na mara nyingi wanajenga mawazo hasi au ya kukanganya kuwahusu wao wenyewe kama hawatapata msaada. Matatizo hayo ni yapi na unawasaidiaje watoto kujenga mawazo chanya wenyewe wakiwa kwenye ulezi?
Angalia video hii juu ya mazungumzo kati ya mlezi na kijana. Kijana ana wasiwasi wa kuwatembelea ndugu zake. Angalia jinsi mlezi anavyomsikiliza kwa makini msichana na jinsi anavyomuelewa hisia zake. Katika mazungumzo mlezi anakuwa anamsaidia vizuri sana msichana kuweza kukabiliana na wasiwasi na kumfanya anaweza kutabasamu.
Wanapowekwa kwenye familia mlezi, mtoto mara nyingi anakutana na mgogoro wa utii: ” Niko karibu na wazazi wangu – lakini wazazi walezi wangu wananijali na kunipenda. Ninawezaje kulipokea hili bila kujisikia hatia au kama msaliti kwa wazazi wangu?”
Mgogoro huu alio nao mtoto unaweza hata kuwa na maumivu zaidi kama wazazi wake wana masuala ambayo hayajatatuliwa ( hasira, wivu) dhidi ya familia mlezi, kwa kuwaona kama mtu aliyeiba moyo wa mtoto wao. Ni vigumu kuamua wengine wamhudumie mtoto wako na vigumu zaidi kama “familia mpya” ina mali zaidi.
Kama ilivyoelezwa kwenye masomo mengine watoto wadogo sana huweza kujenga uhusiano wa karibu na wazazi walezi baada ya muda fulani. Kama hii ikitokea, yamkini mtoto ataanza kukuita “mama” au “baba”. Unaweza kukubali hili ukijua kwamba mtoto atakapokuwa mkubwa atatafuta namna ya kuelewa historia yake mwenyewe. Labda mtoto mdogo au mtoto anayejifunza kutembea atakuchukulia kama mzazi. Lakini lazima ajifunze akiwa na umri mdogo kuelewa kwamba pia ana wazazi halisi. Katika umri wa miaka mitatu au minne kwa kawaida unaweza kuanza kuzungumzia “una jozi mbili za wazazi” Hii inapaswa kufanyika kabla mtoto hajasikia kutoka kwa watoto wengine au watu wazima kwamba ninyi si ” wazazi halisi”.
Hizi hisia asili za wazazi walezi kwa wazazi halisi lazima zitatuliwe – na hii huchukua muda – ili kwamba isimuweke mtoto anayelelewa katika mgogoro mkubwa wa kugawa utii. Ni muhimu kuelewa kwamba hasira au chuki yoyote kwa wazazi itachukuliwa na mtoto kama hasira kwa sehemu ya utambulisho wa mtoto mwenyewe.
Mtoto anayelelewa anaweza kwa hiyari yake kukana au kujaribu kuwasahau wazazi wake, lakini gharama ya hili itakuwa kwamba atagawanyika mwenyewe kwa sehemu moja kuwa na uhusiano wa karibu na wazazi wake na sehemu nyingine uhusiano wa karibu na wazazi walezi, bila kuweza kuwaunganisha hawa wawili kuwa wamoja katika dhana moja iliyo wazi. Hatimaye, hili litakuwa tatizo kwa mtoto, hususani katika umri wa ujana balehe wakati kijana anajaribu kujenga utambulisho wa utu uzima. Kila mara mtoto anapofikia hali mpya ya kukua kisaikolojia na kupata uelewa uliopevuka zaidi kumhusu yeye mwenyewe, lazima ajenge wazo jipya kuhusu utambulisho na historia, hivyo ni mchakato ambao unachukua miaka mingi.
Mitazamo yako kwa wazazi pia ni ujumbe kwa mtoto kuhusu kama anaweza kujiheshimu na kujisikia fahari ya yeye ni nani – mitazamo hasi kwa wazazi itazalisha kujiamini kusiko kuzuri kwa mtoto. Moja ya kazi ngumu kwa mzazi mlezi ni kukuza mtazamo chanya wa kweli wa wazazi ili kumsaidia mtoto.
- Ulipompokea mtoto, ulijisikiaje kuhusiana na wazazi wake?
- Uliona matatizo gani kwa mtoto ambayo yalisababishwa na kukosa ulezi wa wazazi?
- Ulimwelezaje mtoto kuhusu namna unavyowaona wazazi wake?
- Mtoto alikuwa anaelewa nini kuhusu kuwa kwenye ulezi?
- Ni kitu gani kigumu sana kwako katika kuwakubali wazazi au kuona sifa zao nzuri?