Somo la 1/19
Ukurasa 3/5: Mada A: Jinsi ya kutumia programu ya mafunzoMada A: Jinsi ya kutumia programu
Kadi ya maelezo imetengenezwa kukuandaa wewe na mwalimu wako kwa kazi yako ijayo na masomo na kwa kutafakari kwako kuhusu ulichojifunza na namna unavyoandaa mazoezi yako. Kadi ya maelezo ni njia ambayo unatumia – kwa pamoja na mwalimu wako – kukusaidia kuzingatia katika chimbuko la kazi yako ya kila siku ya matunzo ya mtoto. Pamoja na Kadi ya maelezo unaulizwa maswali kadhaa kuhusu malezi ya mtoto, na kujibu maswali ya kadi ya maelezo kutakupa picha ya jumla ya changamoto za watoto na rasilimali, na wazo la kile unachotaka kuboresha katika ulezi wako.
Utakapokuwa umejibu Kadi ya maelezo, utakuwa na wazo zuri kuhusu hali yako halisi, na kitu gani kitakuwa muhimu kufanyia kazi wakati wa masomo.
Tafadhali zingatia: Majibu yako katika mahojiano ya Kadi ya maelezo sio mtihani; ni nyenzo yako kwa ajili ya kuchanganua na kupanga unachoona ni muhimu kukifanyia kazi wakati unatumia programu ya mafunzo. Ni kama kuangalia malezi yako kutoka kwenye mtazamo wa helikopta. Kutokana na mtazamo huo, unaweza kuamua unataka kufanya nini wakati wa mafunzo.
Katika mchakato wa mafunzo haya, utafanyia kazi masomo sita kati ya 15 kwa pamoja na mwalimu wako. Mafunzo yanapangwa kiasi kwamba mwalimu wako anakuongoza katika kila hatua, akikuongezea zaidi katika ujuzi na ustadi wako wa malezi.
Mafunzo yanapokwisha, unakaribishwa kuendelea kujifunza mwenyewe kwa kupitia masomo yaliyobakia.
Kuna nini katika somo? Kila somo linazungumzia mada moja (kwa mfano Somo la 4 linazungumzia: “Kuelewa Nadharia ya Msingi ya Uhusiano wa karibu”) katika maandiko na video ili kukuonyesha uzoefu wa kiutaalamu na nadharia ambayo ni muhimu kuhusiana na mada.
Katika kila somo utatakiwa kutafakari, kufikiria na kupanga namna ya kutumia ulichojifunza. Tunakuomba uwe mbunifu na utafute mawazo yako kuhusu namna unavyoweza kutumia ulichojifunza. Unajua vizuri jinsi ya kutumia maarifa yaliyotolewa katika programu.
Mwishoni mwa kila somo, mwalimu atakwambia kuandika au kukumbuka namna utakavyotumia mawazo na mipango yako hadi mtakapokutana tena katika somo linalofuata.
Tunapendekeza kwamba kama inawezekana weka shajara (diary) – mara nyingi unaweza kuona mafanikio unapotazama nyuma, na unaweza kuwa na seti ya matini zenye manufaa kushirikishana na mtoto unayemlea kadri anavyokua mkubwa. Chochote ulichokiona utakachokiandika au kukirekodi, kisitumike au kuonwa na mtu yeyote ambaye hashiriki katika programu ya mafunzo. Taarifa hizo ni siri.
Hapa kuna mfano wa mkufunzi anayeelimisha kikundi cha wa wakinamama wa SOS. Tafadhali angalia jinsi mkufunzi anavyowashirikisha washiriki na kufanya waongee.