Somo la 2/19
Ukurasa wa 2/4: Upangaji wa mfumo wa maadili mazuri katika familia yakoUpangaji wa mfumo wa maadili mazuri katika familia yako
Kumpokea mtoto wa kulea ni kama vile kujifungua – kuwasili kwa mwanafamilia mpya kunaleta mabadiliko katika majukumu na uhusiano katika familia nzima.
KUIANDAA FAMILIA KWA AJILI YA KUMPOKEA MTOTO WA KUMLEA
Kuna kazi mbili katika kumpokea mtoto aliye katika matunzo:
- kwanza ni kufanya maandalizi ya vitendo kama vile kuamua mtoto atalala wapi.
- Kazi nyingine ni kufanya maandalizi ya kiakili ya namna ya kumsaidia mtoto kujumuishwa katika familia. Hili ni muhimu zaidi kuliko mazingira ya vitendo, na zoezi lifuatalo litakuwa kazi yako ya kwanza ya kitaalamu. Ni kuhusu kutafuta maadili mazuri, ambayo unaweza kumpa mtoto.
Hapa ni video ya Mariam, ambaye amehamia kwa bibi na babu yake baada ya wazazi wake kufariki. Anatugaia mazungumzo juu ya maisha yake katika malezi ya kindugu.