Somo la 3/19

Ukurasa wa 5/6 Mada C: Hofu ya kutenganishwa

Mada C: Hofu ya kutenganishwa – “Alitupenda kuanzia siku ya kwanza- au je alifanya hivyo?”

Mtoto au kijana anaweza kujieleza hofu yake ya kutengana kupitia mielekeo mbalimbali ya tabia.

Baadhi ya watoto hawatapata mahitaji na imani zao na watakuwa tayari kufanya lolote ili kuendana na walezi wapya, ili kuepuka kukataliwa tena. Kwa baadhi, inaweza kuonekana kama baadhi ya watoto wanawapenda wazazi wanaowatunza na wanajirekebisha vizuri kuanzia siku ya kwanza. Inaweza kuonekana kwamba watoto hawa wanaweza kumfikia mtu yeyote wanayekutana naye kwa njia ya ucheshi wa kiwango cha juu. Japokuwa kuunda muunganisho wa kihisia kunachukua muda mrefu. Kwa hiyo, unapaswa kuziona aina hizi za tabia kama njia ya mtoto kuepuka kukataliwa. Tabia hii ya kujirekebisha inasukumwa na hofu ya kutengana. Baada ya miezi michache mtoto ataanza kujihisi yupo salama, na utaweza kushuhudia baadhi ya matatizo na migogoro aliyokuwa nayo mtoto. Ukweli kwamba mtoto anaonyesha aina hii ya tabia ni ishara tosha kwamba mtoto anaanza kujisikia salama na hivyo kukuamini kutomuacha hata kama anaeleza matatizo yake kwako.

Watoto wengine wataonyesha tabia tofauti na hii. Badala ya kuonyesha uwezo mkubwa wa mabadiliko, wanaweza kuonyesha hawaogopi kukataliwa, hivyo kuepuka kuwa na uhusino na walezi wao wapya wote. Watoto hawa mara nyingi wanakabiliwa na tatizo kubwa la kutelekezwa mapema katika maisha, na hivyo wamejifunza hili, ili kutokata tamaa na kukataliwa, ni vizuri kutomtegemea mtu mzima. Kwa mara ya kwanza inaweza kuonekana kwamba mtoto anajitegemea sana na hahitaji msaada wako. Hata hivyo, kumbuka kwamba huu ni ujanja tu wa kuishi na kwamba watoto wote wanahitaji kuendelea kutunzwa, kusaidiwa na kupendwa. Wakati ambapo mtoto anajisikia kulindwa zaidi na wewe na kujifunza kwamba hutamuacha, ataanza kukuamini na kuwa na hisia za kuwa karibu na wewe. Inaweza kuchukua muda mrefu kujenga tena uwezo wa mtoto kuwaamini binadamu wenzie, lakini kila uzoefu mzuri wa mlezi mpya wa mtoto ni hatua ya mwelekeo sahihi.

Kama mtoto alikabiliwa na kutelekezwa mapema, na hivyo kushindwa kujenga uhusiano wa karibu na watu wazima, mara nyingi bila kuhoji na bila kujali mipaka, anaweza kujenga ukaribu na mtu yeyote atakayekutana naye bila kujenga uhusiano wowote wa kina. Inaweza kuchukua miaka kadhaa kujenga uhusiano wa karibu na mtoto wa aina hii. Mwitikio mwingine wa kukosa matunzo ya mapema unaweza kuonekana kwa watoto ambao ni wakimya sana, ambao wanaepuka aina yoyote ya kukutana, na ambao hawaonyeshi uhitaji wowote wa kujenga uhusiano wa karibu (mfano kwa kutoonyesha hisia za kutenganishwa nakupoteza katika hali ambazo hisia zitakuwa za kawaida kwa mtoto au kijana).

MASWALI KWA AJILIYA KUTAFAKARI NA MAZUNGUMZO
  • Upi ulikuwa mwitikio wa kwanza kwa mtoto alipokutana na wewe?
  • Je, unadhani wewe unamsaidia mtoto kujirekebisha kwa kuvumilia na kuhimili?
  • Je, mtoto alionyesha hofu kubwa ya kutengana na wewe? Utakabili vipi hali hii katika njia ya upole na ukarimu linapotokea?
  • Je, mtoto anajaribu kuwa mcheshi na kuendana na matarajio yako – Utafanyaje kwa hili?