Somo la 5/19
Ukurasa wa 4/5 Mada B: Kuandaa mpango kwa ajili ya mazingira yanayochangamsha kwa watoto wachanga na watoto wanaojifunza kutembea katika Mfumo wa Msingi SalamaMada B: Kuandaa mpango kwa ajili ya mazingira yanayochangamsha kwa watoto wachanga na watoto wanaojifunza kutembea katika Mfumo wa Msingi Salama
“Nilikuwa na mtoto. Mara zote alikuwa akitikisa kichwa chake na kulamba nyuma ya mkono wake. Nilihisi kwamba ana mtindio wa ubongo kwa sababu, nilikuwa nimewaona watoto kama hao siku za nyuma. Mara nyingi na kwa uangalifu nilitumia zaidi mbinu nilizojifunza kupitia somo hili kwa mtoto huyu. Sasa, anakaa na halambi tena mkono wake na kutikisa kichwa. Lakini wakati mwingine, anang’ata kucha zake. Hata hivyo, nitaliondoa tatizo hili pia.”
Kauli ya mlezi.
Walezi mara nyingi hawajui namna ambavyo watoto ambao hawakuchangamshwa wanahitaji kuchangamshwa.
Hili linafanya mambo mawili muhimu sana:
- Unawezaje kutengeneza mazingira yanayochangamsha, hususani mchana?
- Unaweza kutumiaje “vifaa vya mama” kuwachangamsha watoto wakati ukiwa huna muda wa kugusana nao kimwili kama ambavyo mama mzazi angefanya?
Sehemu iliyobakia ya somo hili utapata mapendekezo kadhaa kwa ajili ya kufanyia kazi na kwa ajili ya kurekebisha eneo lako la kazi.
Bila shaka utahitaji kurudia hili mara nyingi hadi utakapokuwa umeandaa mazoezi mengine mapya. Unapofanya mabadiliko haya, maisha ya kila siku kidogo yanaweza kuonekana kama yasiyo katika mpangilio na magumu kuyapangilia.
- Tunawezaje kujenga utamaduni ambao mara nyingi tunawakumbatia watoto, kuwapapasa katika njia ya kirafiki mabegani, kuwabembeza huku na huko, kuwashika mkono tunapotembea, na kwa ujumla kuwa na mambo mengi yanayosaidia uhusiano wa karibu wa mwili.
- Mara nyingi unafanyaje unapowabeba watoto, au kuwapakata mapajani? Ni zana gani inaweza kukurahisishia jambo hili, kama vile mbeleko au mfuko wenye kamba unaoweza kuning’inizwa mabegani na mlezi?
- Kitanda kinaweza kuboreshwa kwa njia mbalimbali: kwa kutumia kitambaa cha kinachofyonza maji kama taulo kwa mashuka ambayo huongeza uchocheaji wa ngozi (hakikisha kwamba kitanda hakiwi na joto sana). Unaweza pia kushona na kuweka hamoku kati ya nguzo za kitanda, ili lining’inie juu ya godoro na pia liweze kubembea bila tatizo. Au unaweza kuondoa kitanda kabisa na kutumia mabembea yaliyoning’izwa juu ya magodoro laini yaliyo sakafuni. Vitanda pia vinaweza kubadilishwa ili mtoto aone kinachoendelea wakati anapokuwa macho. Kwa watoto wanaojifunza kutembea unaweza kuweka hamoku juu ya magodoro chumbani au bustanini, na kupanga utaratibu wa kila siku ambapo watoto watafanya zoezi la uchocheaji wenye uwiano.
- Unawezaje kutundika vitu vinavyovutia kwenye vitanda (kama vile simu za mkononi) au badala yake tafuta vitu ambavyo watoto wanaweza kuviangalia wanapokuwa macho vitandani mwao?
- Unawezaje kupiga rangi zinazong’aa na za aina mbalimbali katika kuta na kutundika vitu na picha?
- Unaweza kutumiaje nyimbo na muziki tunaotunga wenyewe? Kuwaimbia watoto na kuimba pamoja na watoto ni muhimu kwa ukuzaji wa lugha. Nyimbo za kubembeleza watoto zina matokeo mazuri mno kwenye ubongo wa mtoto. Karibu kila kitu kinaweza kutumiwa kutoa mapigo kama vile vijiko, ndoo, n.k.